Saturday , November 17 2018

Home / MICHEZO / YANGA YAPIGA MTU 5-1 MOROGORO MECHI YA KIRAFIKI

YANGA YAPIGA MTU 5-1 MOROGORO MECHI YA KIRAFIKI

Yanga Moro 2

Na Mwandishi Wetu
KIKOSI cha Yanga SC leo asubuhi kimeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Tanzanite Centre ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki mjini humo.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mkongo Herithier Makambo, Mrisho Ngasa, Deus Kaseke, Emmanuel Martin na Maka Edward.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya, lakini pamoja na mchezo ujao wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger Agosti 19, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na ile wa mwksho wa dhidi ya Rayon Sport Agosti 28 mjini Kigali, Rwanda.
 Jumapili wiki hii Yanga SC itakuwa na mchezo maalum wa kirafiki wa kumuaga aliyekuwa Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye baada ya kuichezea klabu hiyo tangu mwaka 2006, Cannavaro amestaafu mwishoni mwa msimu uliopita na kuwa Meneja wa timu.
Yanga SC haijashinda mechi hata moja ya Kombe la Shirikisho la Afrika katika kundi lake, baada ya kufungwa mara tatu, mara mbili na Gor Mahia 4-0 Kenya, 3-2 Dar es Salaam, mara moja na USM Alger 4-0 mjini Algiers na sare ya 0-0 na Rayon nyumbani.

About Alex

Check Also

images

RT yamtambulisha mkufunzi kutoka Japan

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), jana limemtambulisha Mkufunzi wa kujitolea kutoka nchini Japan, Ayane Sato. …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eight + twenty =