Wednesday , April 24 2019

Home / Uncategorized / IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI

IDADI YA WANAWAKE WANAOTUMIA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO ZAONGEZEKA NCHINI

DSC_9189

Waziri wa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe.  Penny Mordaunt (katikati) akimsalimia mtoto mchanga aliyebebwa na baba yake katika jengo la Kliniki ya Baba, Mama Na Mtoto. Kulia ni Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. UmmyMwalimu.

DSC_9155

 

Mshauri wa masuala Ya Afya kutoka ubalozi wa Uingereza DKt. Gloria Ngaiza (wapiliKushoto) akimtafasiriaWaziriwa Maendeleo kutoka nchi ya Uingereza Mhe. Penny Mordaunt kilichokuwa kikisemwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tabata (Wa kwanza Kushoto).Wa mwisho Kulia ni Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu.     

Na WAMJW – DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto imesema kuwa idadi ya wanawake wanao tumia huduma za Afya za Kisasa za uzazi wampango zimeongezeka nchini mpaka kufikia Asilimia 32.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo wakati alipoupokea ugeni  wa Waziri wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza katika Zahanati ya Tabata jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kutatua changamoto za Sekta ya Áfya hususani katika huduma za Afya ya mama namtoto.

“Kupitia Msaada wao tumeweza kuongeza idadi ya wanawake wanaotumia huduma za Kisasa za uzazi wa mpango, hatupo vizuri,  tupo Asilimia 32, tumeweka lengo itapofika 2020 tufikie Asilimia 45 ya wanawake walioolewa wanatumia njia hizi” Alisema Waziri Ummy Mwalimu. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi nchini, takribani wanawake 556,000 katika kila vizazi hai laki moja wanafariki na kwamujibu wa Wataalamu uzazi wa mpango utaweza kuchangia Mpaka Asilimia 30 katika Kupungu za vifovitokanavyo na uzazi. 

Pia Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kwa kutenga fedha za ndani katika kupamba na changamoto za sekta ya Áfya ikiwemo kuajiri watumishi wa sekta ya Áfya jambo linalosaidia Kupunguza changamoto hizo za vifo vya akina mama wajawazito na mtoto wa changa. 

“Sisi kama Serikali tumejiongeza, tumechuku hatua na kutenga rasilimali fedha za ndani ikiwemo kuajili watoa huduma za afya, kuhakikisha Kwamba tunatatua changamoto hiyo “alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy aliishukuru Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri wa Maendeleo Mhe. Penny Mordaunt kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za afya hasa katika huduma za mama na mtoto. 

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo kutoka Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameshukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Áfya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi wa Tanzania na kuahidi kupeleka salamu za Tanzania nchini Uingereza.

 

About regina

Check Also

IMG-20180928-WA0022

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI  JESHI la polisi mkoani Pwani, limepiga marufuku kupiga disko toto pamoja …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × one =