Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAVUNDE: KILELE CHA SIKU YA VIJANA DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI ARUSHA AGOSTI 12, 2018

MAVUNDE: KILELE CHA SIKU YA VIJANA DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI ARUSHA AGOSTI 12, 2018

MAVUNDE SIKU YA VIJANA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira), Mh. Anthony P. Mavunde

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira), Mh. Anthony P. Mavunde ameeleza kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kustawi kijamii,kisiasa na kiuchumi.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuujulisha umma wa watanzania kwamba maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Vijana kwa Tanzania yatafanyika mkoani Arusha.

Mh. Mavunde alisema maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 12 Agosti, 2018 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘MAZINGIRA SALAMA KWA VIJANA’

“Natoa wito kwa vijana wote nchini, wazazi na wadau wa Vijana washerehekee siku hii muhimu ili kwa pamoja tuonyeshe na kutambua umuhimu wa vijana kama washiriki wa Maendeleo ya nchi yetu, aidha nawaomba Vijana wote Tanzania wajitokeze na kushiriki katika Maadhimisho haya ili kwa pamoja tuweze kushirikiana na kujadiliana njia na mbinu mbalimbali za kupunguza changamoto zinazowakabili Vijana” alisema Mavunde.

 

About regina

Check Also

4-min

MATUKIO KATIKA PICHA YA WAZIRI KAMWELWE KATIKA KIKAO KAZI KUHUSU KUKWAMA KWA MAKONTENA ZAIDI YA 900 BANDARI YA DAR ES SALAM

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akifafanua jambo mbele ya Wafanyabishara  kutoka Congo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × 2 =