Thursday , December 13 2018

Home / MCHANGANYIKO / DKT TIZEBA AWAHAKIKISHIA WASINDIKAJI WA PAMBA KUJIAMINI SOKO LIPO LA KUTOSHA

DKT TIZEBA AWAHAKIKISHIA WASINDIKAJI WA PAMBA KUJIAMINI SOKO LIPO LA KUTOSHA

 

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni waendeshaji wa soko la bidhaa nchini, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.
Wanunuzi /wasindikaji wa zao la Pamba pamoja na waendeshaji wa soko la bidhaa nchini Tanzania Merchantile Exchange (TMX) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Juzi tarehe 9 Agosti 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano Mwanza Hotel.

Na
Mathias Canal, WK-Mwanza
 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles
Tizeba amewahakikishia wanunuzi na wasindikaji wa zao la Pamba kuendelea
kununua na kusindika pamba kwa wingi kutoka kwa wakulima kwani soko la zao hilo
kwa sasa limeimarika kwa kiasi kikubwa.
 
Waziri Tizeba ametoa kauli hiyo juzi tarehe 9 Agosti 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa kazi kati ya  wanunuzi /wasindikaji
wa zao la Pamba pamoja na Tanzania Merchantile Exchange (TMX) ambao ni
waendeshaji wa soko la bidhaa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza.  
 
Katika mkutano huo uliokuwa na
lengo la kuwapatia uelewa wanunuzi wa zao la Pamba Mhe Tizeba alisema kuwa kuna
njia mbadala zaidi ya waliyonayo sasa ya kuuza Pamba yao katika soko la bidhaa
ambapo bidhaa hushindanishwa kutokana na ubora wake kwa wanunuzi walio wengi
Duniani.
 
Alisema kuingia kwenye ushindani
wa soko ni miongoni mwa njia muhimu na madhubuti kwao kwani itaongeza thamani
ya zao hilo hivyo kuwa na kipato kikubwa kitakachoongeza tija na mafanikio ya
kipato.
 
Tanzania Merchantile Exchange
(TMX) inawakutanisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa kwa pamoja na kwa wingi ili
washindane katika bei jambo ambalo litawafanya wauzaji kuuza bidhaa zao kwa
kiasi kizuri cha fedha na kupelekea kupata bei nzuri.
 
Katika mkutano huo Mhe Waziri wa
kilimo Dkt Charles Tizeba aliwataka wanunuzi hao kujifunza namna ambavyo soko
la bidhaa Tanzania Merchantile Exchange (TMX) linafanya kazi Kwa kupeleka kiasi
cha Pamba kilichozidi kutokana na mkataba walioingia na wanunuzi wao Nje ya
nchi ili kujionea manufaa yaliyopo. 
 
Hata hivyo Mhe Tizeba aliwataka
wanunuzi hao kuendelea kununua Pamba kwa wakulima bila wasiwasi wowote, kwani
soko la bidhaa litaweza kutumika kwa manufaa makubwa kuuza Pamba yao na
kumhakikishia mkulima soko.
 
Alisema kuwa Katika ngazi ya
uzalishaji ni muhimu sana ubora wa pamba ukaimarishwa ili soko la bidhaa liweze
kufanya kazi kwa ufanisi.
 
Aidha, Mhe Tizeba ameilekeza TMX
kukutana na kampuni zinazonunua pamba mmoja mmoja ili kubaini kampuni ambazo
zitaweza kuanza msimu huu kutumia soko la bidhaa.
 

About regina

Check Also

GY3A9651

Mahiga:Tuadhimishe Uhuru kwa kuwakumbuka waliopigania Uhuru huo

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − eleven =