Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / HOSPITAL YA MAFIA YAPATIWA X-RAY ILI KUWAONDOLEA USUMBUFU WANANCHI WALIOKUWA WAKIUPATA KIPINDI CHA NYUMA

HOSPITAL YA MAFIA YAPATIWA X-RAY ILI KUWAONDOLEA USUMBUFU WANANCHI WALIOKUWA WAKIUPATA KIPINDI CHA NYUMA

IMG_20180810_152559

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, mkoani Pwani Ramadhani Maneno akizungumza  wakati kamati ya siasa mkoa ilipofika Mafia na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Mafia ,ambapo kamati hiyo ipo katika ziara ya siku saba kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ilani kuanzia mwaka 2016-2017.(picha na Mwamvua Mwinyi).

IMG_20180810_151934

Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo wakati ,kamati ya siasa mkoa ilipofika Mafia na kuzungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Mafia ,ambapo kamati hiyo ipo katika ziara ya siku saba kukagua miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ilani kuanzia mwaka 2016-2017.(picha na Mwamvua Mwinyi)

NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

TATIZO  la  ukosefu wa  mashine ya mionzi  (X-ray) katika hospitali ya wilaya ya Mafia, mkoani Pwani limepata ufumbuzi wa kudumu baada ya serikali na mbunge kununua mashine mpya ,iliyogharimu sh.milioni 150.#

Ununuzi  wa mashine hiyo ,umesadia kuondoa tatizo walilokuwa wanalipata wagonjwa kutumia gharama kubwa ya usafiri wa ndege kusafirisha kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa vipimo vya mionzi.

Mganga mkuu wa  wilaya ya Mafia, dokta Zuberi Mzige aliyasema hayo, wakati kamati ya siasa  ya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani ,ilipotembelea kisiwa cha Mafia kukagua utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya serikali ya awamu ya tano.

Alisema  ,kati ya fedha za ununuzi wa mashine hiyo sh. milioni 50 zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Mafia na milioni 100 zimetolewa na mbunge wa jmbo la  Mafia Ramadhani Dau. 

Akizungumza baada ya kukagua hospitali hiyo mwenyekiti Wa CCM mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno anasema wameridhishwa na jinsi mkoa huo ulivyotekeleza kwa mafanikio makubwa  ilani ya CCM.

Alieleza, kati ya utekelezaji huo ,imeweza kuboresha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi pamoja na kuimarisha miundombinu ya vituo vya afya ,barabara,maji  na ujenzi wa viwanda.

” Nampongeza mkuu wa mkoa mhandisi Evarist Ndikilo ,mimi nampa jina mkuu wa mkoa wa viwanda ,kiukweli ameinua maendeleo na kukuza sekta ya viwanda bila ubishi”alisema Maneno.

Maneno aliwaomba wananchi wamuunge mkono mkuu huyo wa mkoa kwa juhudi anazozichukua .

Pia aliwaasa mkurugenzi ,mkuu wa wilaya ,madiwani na chama washirikiane kwa kuungana pamoja ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evaristi Ndikilo alifafanua ,katika kipindi hicho zaidi ya vituo saba vya afya vimepatiwa sh.milioni 450 kwa ajili ya upanuzi.

Hata hivyo,Ndikilo alisema, watayafanyia kazi maboresho yote waliyopatiwa na viongozi wa chama mkoa ili kutekeleza ilani zaidi ya sasa na hatimae kupiga hatua kimaendeleo.

About regina

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 8 =