Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dotto James awataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta (TEMCO) Kibaha

Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dotto James awataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta (TEMCO) Kibaha

01

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Dotto James akikata utepe  pamoja na viongozi wengine wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha Mkoani Morogoro kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.

02

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Dotto James akikata wakishangilia mara baada ya kukata utepe  pamoja na viongozi wengine wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.

3

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Dotto James akijaribu kuwasha moja ya Matrekta  yaliyokabidhiwa kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.

4

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Dotto James akizungumza wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo.

5

Dk. Leonard Akwilapo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia akizungumza katika hafla hiyo kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Dotto James

11

Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA mkoani Morogoro wakiwa katika hafla hiyo.

13

Baadhi ya Matrekta yaliyounganishwa tayari kwa kuuzwa.

…………………………………………………………………………………..

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango  Dotto James amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta  yaliyopo katika kiwanda cha kuunganisha matrekta ambacho kinamilikiwa na Serikali kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kuwa matrekta hayo yanaubora wa hali ya juu na kuwahakikishia wananchi watakaoyanunua matrekta hayo kutokuwa na hofu kwani uingizwaji wake Serikali inahusika moja kwa moja.

Katibu  James aliyasema hayo Kibaha mkoani Pwani wakati akikabidhi matrekta kumi kwa Chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi I littles na Rais Dkt.John Magufuli baada ya kufanya ziara  chuoni hapo .

Alifafanua rais alipofanya ziara chuoni hapo alihaidi mambo mawili la kutoa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ahadi ambayo tayari imetekelezwa na jana amekamilisha ahadi ya kukabidhi matrekta hayo.

”  Ninawataka kwenda kutumia vizuri matrekta haya na kuyafanyia matengenezo iwapo yatahitaji matengenezo kwani sisi watanzania hatuna utaratibu wakutuza vitu hata kama tukiona vimeharibika.”alisema James.

Nakuongeza kuwa” Sisi kama serikali tunachombo maalum cha kufatilia fedha na ahadi zote ambazo zinatekelezwa ,hivyo hata matrekta haya tutafatilia kuona yanatumikaje na iwapo  mkitumia vizuri na hata kama.mkiomba zingine tutawapa”alisema James.

Akizungumzia taasisi hizo za fedha  hususani Mfuko wa Pembejeo wa Serikali pamoja na Benki  kuwaeleza wananchi kuwa wanafedha kwa ajili ya kilimo ili waweze kuchangamkia fursa hiyo.

“Kuna huu mfuko wa pembejeo ,huu ni mfuko wa serikali kabisa na tunatoa ruzuku kama ilivyo kwa benki ya kilimo hivyo mjitokeze ili wananchi wajuwe.” alisema James.

Aliongeza kuwa Serikali ya Tanzania na Poland zimeingia makubaliano kwa ajili ya kutengeneza matrekta lengo nikuona tunakuwa na matrekta ya kutosha na kwakuazi ni kutengeneza matrekta 2400  kwa nchi mzima..

Kwa upande wake Makamu mkuu wa Chuo cha Kilimo (SUA)  Profesa Raphael Chibunda  alimhakikishia Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Dotto Kwamba matrekta hayo watayatumia vizuri huku wakishukuru pia kupewa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni.

Alisema kwakuwa chuo chake ndicho ambacho kinatoa watalaamu wengi kwenye kilimo hivyo watahakikisha utaalamu huo unawafikia kikamilifu watanzania kupitia sekta ya kilimo.

About bukuku

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × 5 =