Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUYUNGU YAKAMILIKA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAPIGWA MSASA

MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUYUNGU YAKAMILIKA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAPIGWA MSASA

PICHA - 2

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Uchaguzi katika jimbo la Buyungu (hawapo pichani), wilayani Kakonko wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo leo Agosti 11, 2018.

PICHA - 3

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kiziguzigu Bi. Jesca Masawe akifafanua jambo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wakati wa mafunzo ya kusimamia uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu leo.

PICHA - 4

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ya Kakonko  Bi. Martina Ulungi akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kufunga lakiri (seal) za usalama kwenye maboksi ya kura wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo wilayani Kakonko.

PICHA - 5

Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura wakati wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kusimamia uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu leo.

PICHA - 6

Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya kupigia Kura wakiangalia lakiri (seal) za usalama zinazofungwa kwenye maboksi ya kura mara wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo wilayani Kakonko.

PICHA - 7

Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya kupigia Kura wakifanya mazoezi kwa vitendo ya kufunga vituturi vya kupigia Kura vitakavyowekwa kwenye vituo vya kupigia Kura wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kusimamia uchaguzi mdogo leo wilayani Kakonko.

PICHA - 8

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kakonko wakikagua na kuhakiki majina yao kwenye orodha ya Daftari la Wapiga Kura yaliyobandikwa katika Kituo cha Kupigia Kura cha Ukumbi wa Mikutano wilayani Kakonko leo.

PICHA - 10

Mafunzo kwa vitendo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo jimbo la Buyungu yakiendelea leo katika jimbo la Buyungu.

PICHA -1

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Lusubilo, Kigoma Bw. Joeli Mwakibibi akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo (11 Agosti 2018) wakati wa mafunzo ya Kusimamia uchaguzi  mdogo wa Ubunge utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.

PICHA -9

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko Lusubilo, Kigoma Bw. Joeli Mwakibibi akiwaapisha Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura leo (11 Agosti 2018) ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufuata sheria wakati wa mafunzo ya Kusimamia uchaguzi  mdogo wa Ubunge utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu.

About bukuku

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 × two =