Thursday , December 13 2018

Home / MCHANGANYIKO / MKUU WA SHULE ADAKWA AKIMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI

MKUU WA SHULE ADAKWA AKIMFANYIA MTIHANI MWANAFUNZI

BURUNDI

MWALIMU mkuu wa shule moja nchini Burundi aliyefahamika kwa jina la  Benjamin Manirambona amekamatwa kwa kosa la kumfanyia mtihani mwanafunzi.

Manirambona anadaiwa kudanganya kuwa yeye ni mwanafunzi akiwa na lengo la kumfanyia mtihani mtu mwingine.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na Polisi akiwa kwenye darasa la mtihani ambapo alikuwa akifanya mtihani huo.

Anadaiwa kufahamu kuwa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za raia walikuwa wanamsubiri usiku kucha shuleni hapo ili wamkamate.

Bila ya kuwepo mahala pa kutorokea mwalimu huyo mkuu wa taasisi ya Butere alikiri papo hapo.

Bw Manirambona alieleza kuwa alikuwa akifanya mtihani huo wa niaba ya mwanajeshi aliyekuwa akihudumu nchini Somalia kama sehemu ya kikosi cha Burundi cha kulinda amani. Alisema mwanafunzi alihitaji alama hizo hizo ili apate kujiunga na chuo kikuu.

Chanzo: BBC Swahili.

About regina

Check Also

????????????????????????????????????

Wafanyakazi wa TBL Mbeya na Arusha wapatiwa elimu ya kupinga Ukatili wa kijinsia

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL)  mwaka huu kwa mara nyingine imeungana na mashirika yanayopinga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + seventeen =