Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / WATOTO 5,115 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI TABORA BADO HAJARIPOTI SHULENI

WATOTO 5,115 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MKOANI TABORA BADO HAJARIPOTI SHULENI

1 (7)

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mji Nzega Philemon Magesa jana wakati wa kilele cha juma la elimu kwa Mkoa huo.

2 (9)

Baadhi ya Walimu na Maofisa Elimu wakiwa katika maandamano ya amani jana ya kuhitimisha juma la elimu kwa Mkoa wa Tabora.

7a

.Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari ya Kamagi Hussein Juma (wa pili kutoka kulia) akitumia chura aliyepasuliwa kutoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) kuhusu mfumo wa mmengeyo wa chakula unavyofanyakazi ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha juma la elimu Mkoani humo lililomalizika jana mjini Sikonge.

NA TIGANYA VINCENT

11 AUGUST 2018

JUMLA ya watoto 5,115  kati ya 11,004 ambao walikuwa watoro kwa Shule  za Msingi na Sekondari Mkoani Tabora bado hajaripoti shuleni kama ilivyoagiza viongozi wa Mkoa huo.

Taarifa hiyo ilitolewa jana  mjini Sikonge Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nusu wakati sherehe za kuhitimisha juma la elimu Mkoani humo

Alisema tangu uongozi wa Mkoa huo ulipozindua kampeni ya kuhakikisha watoto wote ambao ni watoro wanarudi shuleni chini ya kauli mbiu ya kamata weka ndani kwa kushindwa kutii amri halali ya Serikali bado kuna baadhi ya watoto hadi hivi sasa bado hawapo shuleni.

Nusu alisema takwimu zinaoonyesha katika Shule za Msingi idadi ya wanafunzi waliokuwa watoro kabla ya kampeni ilikuwa 7,806 lakini baada ya kampeni waliorudi shuleni ni watoto 3,855 ambao ni sawa na asilimia 49.39 na walibaki kuwa  watoro ni 3,951.

Alisema kwa upande wa shule za Sekondari wanafunzi watoro kabla ya kuanza kampeni walikuwa 3,198 ambapo waliorudi shuleni ni 1,260 ambao ni sawa na silimia 39.40 na kubaki idadi ya watoro 1,938.

Nusu alisema jitihada zinaendelea kufanyika ili kuhakikisha watoto wote wa shule za Msingi na Sekondari ambao bado hajarudi shule wanasakwa popote walipo ili warudishwe darasani na wazazi wao wachukuliwe hatua.

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa ukuzaji wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) alisema katika Mkoa wa Tabora takwimu za wanafunzi wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu zimekuwa zikipungua kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wazazi ,viongozi na walimu katika shule mbalimbali.

Nusu alisema takwimu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018 jumla ya watoto 21,288 walikuwa hajuia KKK na hadi kufikia Mwezi Agosti mwaka huu idadi imepungua na kufikia 11,399 ambao hawajui Kusoma, Kuandika na kuhesabu sawa na asilimia 54.

Aidha Afisa Elimu huyo wa Mkoa alisema hali ya utoaji wa chakula shuleni imekuwa ya kususua kwani tangu shule zilipofunguliwa ni Shule za Msingi 232 kati ya 769 sawa na asilimia 30.2 ndio zilikuwa zikitoa chakula kwa wanafunzi.

Kwa upande wa Sekondari alisema shule 95 kati ya 154 ambazo ni sawa na asilimia 61.8 ndio zinatoa chakula kwa wananfunzi.

Alisema hali hiyo haridhishi kwani tendo la kujifunza linahitaji afya ya mwili wenye lishe bora ili mwanafunzi aweze kujifunza vizuri na kutoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanasaidia watoto wao.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuanza kuwachukulia hatua wazazi, viongozi wakiwemo Maofisa Elimu Kata walioshindwa kuhakikisha watoto watoro katika maeneo yao wanarudi mara moja shule.

Alisema hatua hizo ni pamoja na kuwakamata wazazi wa watoto watoro na kuwaweka ndani na kuwavua vyeo wale  Maofisa Elimu Kata ambao maeneo yao itaonekana utoro umeshamili kwa sababu ya  kushindwa kutimiza wajibu wao kama wasimamizi wa masuala ya elimu kwa ngazi za Kata wakati usafiri wanao.

Mwanri alisema haiwezekani washindwe kuwakamata wazazi wa watoto watoro wakati majina ya watoto hao na wazazi wao alishawapa kupitia Ofisi ya Elimu Mkoa na pia wao wanaishi nao.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema jirani wa mzazi wa mtoto mtoro atakamatwa kama atashindwa kutoa taarifa katika Ofisi husika kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamtaka kila raia kuhakikisha anafichua uovu anapouona.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alisema uchunguzi uliofanywa Wilayani humo umeonyesha kuwa utoro mwingine umesababisha na watoto kulelewa na bibi zao kwani mabinti wanapojifungia wanawaacha kwa wazazi wao na kuondoka. 

Alisema watoto hao kwa kubaki na bibi zao wakati mwingine wanakosa mahitaji kwa ajili ya shule na wakati mwingine mtu wa kuwahimiza kwenda shule. 

Naye Ofisa kutoka Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) Salum Mkuya aliwashauri Walimu kuweka vivutio mbalimbali kama vile kuwa na kwaya, michezo, gwaride , mcahakachaka na michezo mengine kwa ajili ya kuwavutia watoto kupenda kuwepo katika mazingira ya shule. 

Alisema hatua hiyo itasaidia sio tu kuwavutia bali hata kuibua vipaji wa watoto na kujenga uzalendo wa kuipenda Nchi wakiwa watoto na vijana wadogo. 

Juma la elimu liliadhimishwa kuanzia tarehe 5 hadi 10 Agosti mwaka ambapo kauli mbiu yake ilikuwa Ukuzaji wa stadi za KKK Tabora inawezekana kila mmoja atomize wajibu wake.

 

About regina

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − 11 =