Friday , October 19 2018

Home / SIASA / MADIWANI WAWILI CUF MAFIA WARUDI CCM LEO

MADIWANI WAWILI CUF MAFIA WARUDI CCM LEO

IMG_20180812_143505

Aliyekuwa diwani wa Jibondo wilayani Mafia Hassan Mohammed  Hassan ,akimpa mkono Mwenyekit wa Chama Cha Mapinduzi,Mkoani Pwani Ramadhani Maneno baada ya  kujihudhuru nyadhifa yake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi)

NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA
MADIWANI wawili kutoka chama cha wananchi (CUF) kata ya Kilindoni na Jibondo ,wilayani Mafia ,Mkoani Pwani, wamejihudhuru nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,kutokana na chama tawala kurudisha heshima na kuwa sikivu nchini.
Madiwani hao wamerudi CCM katika ziara ya kamati ya siasa mkoani Pwani ,iliyoweka kambi siku mbili wilayani humo,kutembelea miradi na kukagua utekelezaji wa chama hicho .
Aliyekuwa diwani wa Jibondo Hassan Mohammed  Hassan ,alisema amefanya maamuzi hayo kutokana na chama walichokuwepo kukosa mwelekeo na kukosa sera zinazojiuza.
Alisema ,kata ya Jibondo ilikuwa na wafuasi wa CCM ambapo ilipofika 2004 wengi wao walihamia upinzani kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda wanavyotaka.
“Nampongeza Rais Dk.Magufuli, mkuu wa mkoa wa Pwani, wilaya na CCM Mafia na mkoa kwa juhudi zao katika kuinua uchumi wa nchi na kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji” alibainisha Hassan.
Nae aliyekuwa diwani wa Kilindoni ,Ahmad Mbonde,alisema hajanunuliwa kwani kata yake ipo mjini, ilikuwa tishio na ilitikisa .
“Leo hii nafanya maamuzi haya ,kwa akili zangu ,pasipo kushawishiwa bali ni kutokana na serikali kufikisha fedha nyingi kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo bila ubaguzi “
“Serikali hii ni sikivu na imesaidia mengi katika kata zetu hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya afya ,elimu ,maji na kusikiliza wanyonge” alisisitiza Mbonde.
 
Akiwapokea madiwani hao,mwenyekiti wa CCM Pwani,Ramadhani Maneno alisema hawajafanya makosa kurudi CCM.
Alielezea inaashiria tosha kuwa CCM ya sasa na mpya kwani inakubalika na wananchi,wasio wana CCM na viongozi wa upinzani ambao wanakimbia vyama vyao kila uchao.
Awali mkuu wa wilaya ya Mafia ,Shaibu Nnunduma alisema walikwenda ofisini kwake kuomba kurudi CCM bila kushawishiwa.

Alisema ushirikiano baina ya mbunge,CCM wilaya ,halmashauri na wilaya pamoja na ngazi za Taifa imewasukuma madiwani hao hivyo aliomba ushirikiano huo uendelee.

 

About regina

Check Also

IMG_20181014_112001_199

HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI

 Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akimkabishi chetu mbunge mteuliwa wa Jimbo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 + 6 =