Wednesday , December 12 2018

Home / MCHANGANYIKO / MTALII AUAWA HUKU MWENZAKE AKINUSURIKA KIFO BAADA YA KUVAMIWA NA KIBOKO WAKATI WAKIMPIGA PICHA

MTALII AUAWA HUKU MWENZAKE AKINUSURIKA KIFO BAADA YA KUVAMIWA NA KIBOKO WAKATI WAKIMPIGA PICHA

KIBOKO

Mtalii kutoka China, Chang Ming Chuang amefariki dunia huku mwenzie aliyefahamika kwa jina la Wu Peng Te akinusurika kifo baada ya kujeruhiwa na kiboko wakati wakimpiga picha.

Mamlaka ya hifadhi ya wanyamapori nchini Kenya imesema mkasa huo ulitokea jana katika ziwa Naivasha lililoko eneo la Sopa Resort mjini Nakuru.

Pia, imesema Peng Te aliyenusurika kifo, yuko hospitalini kwa ajili ya matibabu ya majeraha aliyopata.

Marehemu Chuang aliyekuwa na umri wa miaka 66 na Peng Te (62) walikuja nchini Kenya kwa ajili ya kufanya utalii.

Chanzo: BBC Swahili.

About regina

Check Also

1

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akishiriki ‘Msaragambo’ wa ujenzi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seventeen − fourteen =