Sunday , August 19 2018

Home / MCHANGANYIKO / NAIBU WAZIRI MAVUNDE ABAINISHA MIKAKATI YA SERIKALI JUU YA UWEZESHWAJI KIUCHUMI VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ABAINISHA MIKAKATI YA SERIKALI JUU YA UWEZESHWAJI KIUCHUMI VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU

IMG-20180812-WA0156

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde  amebainisha dhamira na mikakati ya serikali katika kuhakikisha inaweka mazingira salama ya kuwawezesha Vijana na Watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuhamasisha makundi mengi ya Vijana kujisajili ili kuunganishwa na fursa za uwezeshwaji kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani na mifuko ya uwezeshwaji wananchi kiuchumi Nchini.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho wa siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu,Tengeru-Arusha ambapo pia ameeleza juu ya mpango wa ukuzaji Ujuzi kwa Vijana ambapo mwaka huu wa fedha 2018/2019 Serikali imetenga Bilioni 15 kwa ajili ya kuwajengea ujuzi vijana wa Tanzania.
IMG-20180812-WA0159
Aidha akitoa maelezo ya awali,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Mashaka Gambo amewataka Vijana kutumia muda wao vizuri kwa kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda wao kufanya mambo yasiyokuwa na tija.
Wawakilishi wa UNFPA na ILO nchini Bi Jaqueline Mahon na Bw Wellingtone Chibebe wameipongeza Serikali ya Tanzania katika programu yake ya Ukuzaji ujuzi na kuahidi kushirikiana na  serikali katika utekelezaji wa mipango hiyo.
IMG-20180812-WA0158
 

About regina

Check Also

efm-2

RC MAKONDA ANOGESHA TAMASHA LA BURUDANI LA ‘KOMAA CONSERT 2018’ LILILOANDALIWA NA EFM

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia maelfu ya wananchi waliofika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × three =