Wednesday , December 12 2018

Home / MCHANGANYIKO / NBC WAKALA YAZIDI KUSAMBAA NCHINI HUKU BENKI IKIDHAMINI MAONYESHO YA NANENANE SIMIYU, MKURUGENZI NAYE ATEMBELEA MIKOA KUANGALIA FURSA ZA KIBIASHARA

NBC WAKALA YAZIDI KUSAMBAA NCHINI HUKU BENKI IKIDHAMINI MAONYESHO YA NANENANE SIMIYU, MKURUGENZI NAYE ATEMBELEA MIKOA KUANGALIA FURSA ZA KIBIASHARA

01 (2)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Athony Mtaka (wa tatu kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi ya wakala mkuu wa huduma ya NBC Wakala mjini Bariadi mkoani Shinyanga hivi karibuni. Wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi pamoja na baadhi ha viongozi wa mkoa huo waliohudhuria hafla hiyo.

02 (3)

 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi (wa pili kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia) pamoja na ujumbe wake walipofika ofisini kwake kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kibiashara katika mikoa ya kanda ya ziwa hivi karibuni.

03 (3)

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jambo Food Products, Salum Khamis maarufu kama ‘Salum Mbuzi’ walipomtembelea kiwandani hapo akiwa pamoja na na baadhi ya maofisa wa benki hiyo.

04 (3)

Mkuu wa Mkoa wa Sinyanga, Zainabu Tellack (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Ltd, Theobald Sabi (wa tatu kushoto), alipomtembelea ofisini kwake, mkoani humo hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni  Mkuu wa kitengo  cha Uhai wa Wateja wa benki hiyo, Gaudence Shawa na Meneja Mahusiano, William Kallaghe.

05 (2)

 Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto), wakifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia), wakati wa mapokezi ya rais mstaafu huyo alipokwenda mkoani Simiyu kufunga maonyesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani humo.

07 (2)

Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa, akikabidhi kikombe kwa Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe kufuatia ushindi wa pili wa benki hiyo katika kitengo cha taasisiza fedha wakati wa maonyesho ya Nanenane mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na kushoto kabisa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo.

 

About regina

Check Also

1

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akishiriki ‘Msaragambo’ wa ujenzi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

10 + seven =