Wednesday , April 24 2019

Home / MICHEZO / WAZIRI LUGOLA AZINDUA BONANZA LA KUTANGAZA AMANI NCHINI

WAZIRI LUGOLA AZINDUA BONANZA LA KUTANGAZA AMANI NCHINI

PIX 2 (9)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto aliyechuchumaa) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Mpira wa miguu ya Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoani Mara mara baada ya Waziri huyo kulizindua Bonanza la Amani linalotarajiwa kufanyika nchi nzima. Bonanza hilo ambalo lengo kuu ni kutangaza amani na utulivu nchini, linajumuisha wachezaji wa mpira wa miguu, wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PIX 1 (9)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Kangi Lugola akizungumza na Wanamichezo pamoja na wananchi wa mjini Bunda wakati analizindua Bonanza la  Amani katika Uwanja wa mpira wa miguu wa Sabasaba, mjini humo leo. Bonanza hilo ambalo lengo kuu ni kutangaza amani na utulivu nchini, linatarajiwa kufanyika nchi nzima likijumuisha wachezaji wa mpira wa miguu, wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amezindua Bonanza kubwa la amani katika uwanja wa mpira wa Sabasaba, mjini Bunda mkoani Mara.

Bonanza hilo ambalo linatarajiwa kufanyika nchini nzima limezinduliwa mjini Bunda na baadae litafanyika nchini nzima likiwa na lengo kuu kutangaza amani nchini.

Akizungumza kabla ya kulizindua Bonanza hilo, Waziri Lugola alisema, michezo inaleta amani michezo inaleta ushirikinao, michezo inaimarisha undugu, michezo inaimarisha ushikamano na michezo uepusha wananchi wasijiingize katika uhalifu, hivyo Wizara yake inatarajia Bonanza hilo litazidi kudumisha amani zaidi.

“Michezo ikiimarishwa tunaimarisha amani, tukishiriki michezo kama hivi wanaokuja kutazama na nyie mnaocheza,  hivyo muda mwingi tunautumia katika kufurahi pamoja na ndio mana vitendo vya uhalifu vitapungua kwasababu watu tunataka tuwe wamoja kupitia michezo,” alisema Lugola. 

Waziri Lugola aliongeza kua, Bonanza la kuhubiri amani sio kwamba linafanya wilyani Bunda bali litafnyika nchi nzima likiwa na lengo la kuwaweka watanzania pamoja ili amani nizidi kudumu. 

“Hapa tulipo ni uwanja wa CCM na hii ilani ni ya CCM na katika ibara ya 160, 161 na 162 inazungumzia kuimarisha na kudumisha sekta ya michezo, hivyo tupo hapa kutokana na ilani hii ya CCM na lengo kuu ni kudumisha amani,” alisema Lugola.

Waziri Lugola yupo wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ndany ya jimbo lake la Mwibara wilayani humo.

About regina

Check Also

1

Wizara ya Habari yawasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/20

 Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seventeen + eighteen =