Friday , January 18 2019

Home / MICHEZO / MO SALAH ACHUNGUZWA NA POLISI

MO SALAH ACHUNGUZWA NA POLISI

mo salah 2

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ‘Mo Salah’ anachunguzwa na polisi nchini England kutokana na kuendesha gari huku akiwa anatumia simu.

Mo Salah ambaye ni raia wa Misri ameingia kwenye mkasa huo baada ya video yake inayo muonyesha anaendesha gari huku akitumia simu, kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Klabu ya Liverpool inadaiwa kutoa taarifa za video hiyo polisi, ambapo msemaji wake amesema kabla ya kuwafahamisha polisi, walizungumza na Mo Salah.

Vile vile, Jeshi la Polisi mjini Merseyside limethibitisha kupokea taarifa za video hiyo na kwamba umepelekwa katika kitengo husika kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

 

About regina

Check Also

hqdefault

SIMBA SC KUONDOKA LEO BILA BOCCO KWENDA DRC KUWAFUATA AS VITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco hatasafiri …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + 14 =