Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / BALOZI DKT. ABDALLAH POSSI ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUJA TANZANIA KWANI INA MAZINGIRA MAZURI

BALOZI DKT. ABDALLAH POSSI ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUJA TANZANIA KWANI INA MAZINGIRA MAZURI

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dtk.Abbdalaah Possi akiwa katika maonyesho ya Gaiexpo mjini Tubingen,mwaka huu nchi lengwa ilikuwa Tanzania

BALOZI wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi amewataka wakezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza hapa nchini kwani kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

Dkt. Possi ametoa wito huo katika maonyesho ya ‘International Afrika Festival’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya International Afrika Festival Tübingen nchini Ujerumani.

Balozi wa Tanzania nchini Ujermani Mhe.dtk.Abdallah Possi akiwa na wawekezaji wakiangalia naadhi ya bidhaa katika maonyesho mjini Tubingen,Ujerumani

Onyesho lilifana sana sana na kuitanga za Tanzania kimataifa ambalo lilikuwa katika viwanja vya maonyesho ya International Afrika Festival Tübingen nchini ujerumani ambapo katika maonyesho hayo mwaka huu 2018 nchi lengwa ilikuwa ni Tanzania na mgeni wa heshima rasmi alikuwa balozi wa Tanzania nchini ujerumani mheshimiwa dkt.Abdallah Possi ambaye alihutubia ummati wa kadamnasi ya waudhuriaji wakiwemo wawekezaji kuwa Tanzania kuna fursa kubwa za uwekezaji na pia nchi salama. 

onyesho hilo kubwa lilinogeshwa na bendi za muziki kama Ngoma Africa band maarufu FFU-Ughaibuni inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi ya Mvula-Mandondo Band inayoongozwa na msanii Saidi Kanda yenye maskani kule Uingereza nayo ilifanya vizuri,wasanii wa kizazi kipya kama Nashi MC kutoka Tanzania naye alitingisha jukwaa msanii wa picha za kuchora Chilonga Haji naye alikuwa moja ya waonyeshaji wa bidhaa toka Tanzania.

 

About regina

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

15 + 19 =