Saturday , March 23 2019

Home / SIASA / CCM YATOA UFAFANUZI KUHUSU MCHAKATO ULIOTUMIKA KUWAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE WALIOTOKEA UPINZANI

CCM YATOA UFAFANUZI KUHUSU MCHAKATO ULIOTUMIKA KUWAPITISHA WAGOMBEA UBUNGE WALIOTOKEA UPINZANI

BASHIRU

Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally.

KATIBU Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ametoa ufafanuzi kuhusu mchakato uliotumika kupitisha majina ya wagombea ubunge waliotoka upinzani na kujiunga katika chama hicho hivi karibuni.

Takribani wabunge watano kutoka vyama vya upinzani hivi karibuni walihamia CCM na wanne kati yao kuteuliwa tena na chama hicho kugombea katika majimbo waliyotoka, wakiwemo aliyekuwa mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara na aliyekuwa Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga.

Akizungumza katika kituo kimoja cha luninga leo tarehe 15 Agosti , 2018, Dkt. Bashiru ameeleza kuwa, CCM haijakiuka katiba yake kwa kuwapitisha wagombea hao pasipo kufanyika kura ya maoni, akisema kuna kanuni zinazoruhusu Kamati Kuu kuamua kura za maoni ziwepo au zisiwepo.

“Tuna kanuni zinazoongoza katiba na kanuni hizo mtu akizisoma vizuri atabaini kuwa kuna wakati kamati kuu inaweza kuamua kura za maoni ziwepo au zisiwepo, la kwanza, lakini pia kuna mazingira ya kura ya maoni ambapo lazima kuwe kuna ushindani ili ushinde, pale hakuna mtu aliyechukua fomu zaidi ya Mwita utalazimisha kura ya maoni? Nenda pale Ilala ambako ndiko chombo cha uongozi cha chama wanasimamia kura za maoni  uliza waliojaza fomu wangapi?  Akijaza mmoja ujue hakuna kura ya maoni.  

Monduli nenda wilayani uulize waliochukua fomu ni wangapi ni Kalanga peke yake. Sasa ikishatokea hali hiyo vikao vinakaa ikikuta huyo hafai wanaitisha utaratibu mwengine, badala ya kura ya maoni sasa vikao ndiyo vinamchuja na kumpa alama na Mwita alipata alama b, ambayo ni alama ya juu na wameridhika na mchango wake na sifa yake, si mla rushwa anakubalika wakamteuwa wakampeleka kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam, nayo ikapelekewa jina moja na kuliteua tukaletewa jana na kamati kuu tukampitisha,” ameeleza Dk. Bashiru.

About regina

Check Also

Kiapo

LOWASSA APOKELEWA KWA KISHINDO MONDULI LEO, AAPISHWA KUWA MWANACHAMA MTIIFU WA CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza jambo na  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × five =