Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / Mdau wa maendeleo wilayani Chemba Khamis Mkotya aombewa dua

Mdau wa maendeleo wilayani Chemba Khamis Mkotya aombewa dua

MKO1

Mkazi wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali, akiwa amemshika kichwa mdau wa maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua na kumshukuru baada ya kufanikisha familia hiyo na nyingine zaidi ya tano kijijini hapo kulipwa fidia ya mashamba yao yaliyokuwa yamechukuliwa na mkandarasi wakati wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati.

Wananchi hao walikata tamaa mwishoni mwa mwaka juzi kutokana na kufuatilia malipo yao bila mafanikio. Mkotya aliguswa na kero hiyo hivyo aliamua kushirikiana nao na kuwapigania hadi walipolipwa stahiki zao. Juzi wakati Mkotya akitoka Dodoma kwenda Kondoa aliamua kupita kijijini hapo ndipo familia hiyo ilipomkaribisha nyumbani ili aone matunda ya kazi yake ya kuwapigania.

Familia hiyo ilimweleza Mkotya kuwa inayofuraha kubwa, kwani fedha walizopata wameweza kununua mashamba mengine na kujenga nyumba bora ya bati (inayoonekana nyuma). kulia ni nyumba ya tembe waliyokuwa wakiishi awali.

MKO2

About bukuku

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × three =