Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / ECLAT FOUNDATION YAKABIDHI SHULE KWA SERIKALI

ECLAT FOUNDATION YAKABIDHI SHULE KWA SERIKALI

IMG-20180819-WA0019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi (Elimu) Toxin Nzunda na Mwenyekiti wa shirika la ECLAT Foundation Peter Toima wakinyanyua juu hati ya makabidhiano ya shule mpya ya msingi Ormotoo ya Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

IMG-20180818-WA0058

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi (Elimu) Toxin Nzunda akizungumza baada ya shirika la ECLAT Foundation kuikabidhi serikali majengo ya shule mpya ya msingi Ormotoo ya Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

IMG-20180818-WA0059

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi (Elimu) Toxin Nzunda akizungumza baada ya shirika la ECLAT Foundation kuikabidhi serikali majengo ya shule mpya ya msingi Ormotoo ya Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

IMG-20180819-WA0016

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi (Elimu) Toxin Nzunda akishukuru baada ya kuvishwa mavazi ya jadi na wananchi wa Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

IMG-20180819-WA0017

Wanafunzi wa shule ya msingi Ormotoo Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakipokea zawadi ya vifaa vya kusomea ikiwemo rula, kalamu, madaftari, penseli, kalamu ya wino na vifutio.

IMG-20180818-WA0067

Wanafunzi wa shule ya msingi Ormotoo ya Kijiji cha Loiborsoit A Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye shule hiyo iliyojengwa na shirika la ECLAT Foundation kwa gharama ya shilingi milioni 201.

Shirika la ECLAT Foundation limeikabidhi Serikali majengo ya shule ya msingi Ormotoo, Kijiji cha Loiborsoit A, Kata ya Emboreet Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara ya thamani ya shilingi milioni 201 yatakayowanufaisha wanafunzi wa jamii ya kifugaji wa eneo hilo.

Akipokea majengo hayo kwa niaba ya Serikali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, (elimu) Toxin Nzunda amelishukuru shirika la ECLAT Foundation kwa kufanikisha mradi huo.

Nzunda alisema shirika la ECLAT Foundation linapaswa kuungwa mkono kwani kwenye maisha hakuna jambo la msingi kama kuwekeza kwenye elimu.

Alisema shirika hilo linashirikiana na serikali katika kuboresha elimu ndiyo sababu wakafanikisha ujenzi huo wa shule hiyo ambayo itawanufaisha wanafunzi wa jamii ya eneo hilo.

Mwenyekiti wa shirika la ECLAT Foundation, Peter Toima alisema ujenzi huo umehusisha vyumba nane vya madarasa, ofisi tatu za walimu, chumba kimoja nadhifu cha wasichana, matundu 24 ya vyoo na vifaa vya kufundishia.

Toima alisema ECLAT Foundation imefanikisha ujenzi huo kwa kushirikiana na shirika la Upendo Society la nchini Ujerumani.

Alisema pamoja na kufanikisha ujenzi huo pia wamekabidhi madawati 179, meza 10, viti tisa na vifaa mbalimbali vya kujifunzia wanafunzi ikiwemo vifutio, penseli, kalamu za wino na madaftari.

Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara, Missaile Mussa alilipongeza shirika la ECLAT Foundation kwa namna wanavyowajali wananchi wa eneo hilo kwani wamewekeza kwenye elimu kwa ajili ya kusaidia jamii ya Simanjiro kupata elimu bora.

“Sisi kama serikali ya ngazi ya mkoa tutaendelea kushirikiana nao ECLAT Foundation kwa ajili ya manufaa ya wananchi wetu wa hapa Simanjiro,” alisema¬† Mussa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akizungumza wakati wa kukabidhiwa shule hiyo aliahidi kuendelea kutunza miundombinu na mazingira wakati huu ambapo wanaimiliki.

Ofisa Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Zuwena Omary akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alisema wanashukuru kwa kutembelewa na Nzunda na wanamkaribisha kwa mara nyingine arudi tena wilayani humo.

About regina

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

6 + 9 =