Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / MAGEREZA YAKUTANA NA WATAALAM WA UREKEBISHAJI KUTOKA SWEDEN

MAGEREZA YAKUTANA NA WATAALAM WA UREKEBISHAJI KUTOKA SWEDEN

PIX 1 (3)

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike, Makamishna  pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu wakisikiliza maelezo ya Bw. Dru Allen (mwenye shati la draft)  kutoka Taasisi ya Roul Wellenburg ya Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden baada ya kukamilisha  ziara ya siku tatu ya kutembelea baadhi ya magereza na Chuo Cha Taaluma ya Urekebishaji  ili kuona na kufanya tathmini ya mahitaji ya kimafunzo kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza nchini.

PIX 2 (3)

Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia maelezo ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati meza kuu) leo Septemba 14, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Magereza katika tukio la kupokea taarifa ya ziara ya Bw. Dru Allen na Terry Sawatsky (mwenye koti)  kutoka Taasisi ya Roul Wellenburg ya Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden, baada ya kukamilisha ziara ya siku tatu katika baadhi ya maeneo ndani ya Jeshi la Magereza.

PIX 3 (3)

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike akipata maelezo kutoka kwa Bw. Terry Sawatsky  pamoja na Bw. Dru Allen(hayupo pichani)  kutoka Taasisi ya Roul Wellenburg ya Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden,  walipofika Makao Makuu ya Magereza  leo Septemba 14, 2018 kujitambulisha kwa maafisa waandamizi wa Jeshi hilo na kutoa mrejesho wa ziara yao ya siku tatu iliyowafikisha katika baadhi ya magereza mkoani Morogoro na Chuo Cha Taaluma ya Urekebishaji (TCTA) ili kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na mtaala unaozungatia Haki za Binadamu kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza.

PIX 4 (2)

Bw. Dru Allen kutoka Taasisi ya Roul Wellenburg ya Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden akipokea zawadi kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike alipofika Makao Makuu ya Magereza baada ya kuhitimisha ziara katika baadhi ya maeneo yaliyo chini ya Jeshi la Magereza ili kufanya tathmini ya kimafunzo ya urekebishaji na mitaala inayozingatia mahitaji ya Haki za Binadamu ndani ya Magereza.

PIX 7 (1)

Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Phaustine Kasike (katikati waliokaa), Makamishna, viongozi waandamishi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu wakiwa katika picha ya  pamoja na Bw. Dru Allen (wa pili kulia) na  Bw. Terry Sawatsky  (wa pili kushoto)  kutoka  Taasisi ya Roul Wellenburg ya Chuo Kikuu cha Lund nchini Sweden. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Uwesu Ngarama na wakwanza kulia ni Kamishna wa Miundombinu na Uzalishaji Tusekile Mwaisabila.

PIX 6 (1)

About regina

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 − 9 =