Wednesday , April 24 2019

Home / BURUDANI / Major Lazer waelekeza tena nguvu Afrika, wamshirikisha Burna Boy

Major Lazer waelekeza tena nguvu Afrika, wamshirikisha Burna Boy

MAJOR

Watayarishaji wa muziki na Madj wenye makazi yao nchini Marekani, Major Lazer wameachia ngoma mpya ‘All My Life’ waliyomshirikisha staa wa Nigeria, Burna Boy. Wimbo huo umekuja na video yake iliyofanyika Lagos na kuongozwa mtengezaji wa filamu wa Afrika Kusini, Adriaan Louw.

Tazama video yake hapa: https://www.youtube.com/watch?v=IW4KbVdISps

Major Lazer wataachia ngoma zingine wakiwashirikisha wasanii wa Afrika kuanzia mwezi September. Bendi hiyo pia itaanza ziara yake kuanzia mwezi huu September na October wakipita katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Ethiopia na Uganda.

Wakiwa Afrika, Major Lazer watafanya kazi na shirika la VETPAW (Veterans Empowered to Protect African Wildlife) kupambana na uwindaji haramu Afrika na kwingineko.

“All My Life” ni wimbo wa kwanza toka kwa mastaa hao tangu walipoachia EP yao, Know No Better mwaka jana.

Major Lazer inaundwa na mtayarishaji wa muziki, Diplo na MaDJ Jillionaire na Walshy Fire. 

HII NDIO RATIBA YA MAJOR LAZER LIVE

September 29 Johannesburg, South Africa    H2O – Wild Waters Complex

September 30 Leopards Bay, Malawi            Lake of Stars Festival

October 5        Lagos, Nigeria Summer Stance

October 6        Nairobi, Kenya            Tuborg Open & Kenya Nights

October 7        Addis Ababa, Ethiopia Bira Biro

October 8        Kampala, Uganda       5th Street Industrial Arena

 

About regina

Check Also

EPSON MFP image

MSANII DAVID JEMS KUTUMBUIZA MASHABIKI WA NGUMI SIKU YA PASAKA DAY MAGOMENI

Na Mwandishi Wetu ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya mpambano wa masumbwi uliokuwa ukisubiliwa kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − one =