Saturday , November 17 2018

Home / MCHANGANYIKO / TAKUKURU YATANGAZA ZAWADI NONO KWA MWANANCHI ATAKAYESAIDIA KUPATIKANA KWA HANSPOPE NA FRANKLIN LAUWO KWA KOSA LA UDANGANYIFU

TAKUKURU YATANGAZA ZAWADI NONO KWA MWANANCHI ATAKAYESAIDIA KUPATIKANA KWA HANSPOPE NA FRANKLIN LAUWO KWA KOSA LA UDANGANYIFU

 

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo akiongea na wanahabari jijini Dar es salaam leo

…………………
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) imewataka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope na Frankline Lauwo kujisalimisha katika ofisi zake au kituo cha polisi kujibu tuhuma zinazowakabili.
Akizungumza na Waandishi wahabari jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo amesema Mshatakiwa wa kwanza Zacharia Hanspope aliondoka nchini mnamo April 8, 2018 kupitia mpaka Horohoro kwa kutumia Passport namba TA00422.
 Amesema kuwa mshatikiwa namba moja anashtakiwa kwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi K/F106(1)(A)&(C) Cha kodi ya mapato chini ya sharia ya kodi namba 332.R.E 2008 kwamba kati ya washtakiwa wenzake Evans Aveva na Godfrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania.Amesema kuwa maelezo hayo yalikuwa kwamba Simba S.C wamenunua nyasi bandia kutoka kampuni ya Ninah Guanzhou Trading Limited kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577.00 USD, maelezo ambayo yalikuwa ya uongo kwania nyasi hizo zilinunuliwa kwa 109,499.00 USD.

Generali Mbungo alisema Franklin Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi bila ya kusajiliwa K/F22(1)(D) Cha usajili wa wakandarasi Sura ya 235 ya 2002 Kwamba kati ya Machi 2016 na Septemba 2016 Mshatakiwa alifanya kazi za ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba Sports Club Uliopo Bunju Manispaa ya Kinondoni kwa thamani ya Tsh 249,929,704 wakati akiwa hajasaliwa katika bodi ya wakandarasi Tanzania hivyo kisheria alikuwa haruhusiwi kufanya kazi hiyo.

 

Aidha, TAKUKURU imetangaza zawadi nono kwa mwananchi atakayefanikisha kupatikana kwa Hans Pope na  Lauwo baada ya TAKUKURU kuwatafuta kwa njia za kawaida bila mafanikio.

About Alex

Check Also

IMG_5910

MAZOEZI YA PAMOJA YA MAJESHI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAMEWAPA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA MBALIMBALI

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × two =