Wednesday , April 24 2019

Home / MCHANGANYIKO / UBALOZI WA CHINA NCHINI WAMKABIDHI ZAWADI YA PIKIPIKI 10 MKURUGENZI WA TAASISI TA TULIA TRUST KWA AJILI YA WASHINDI WA TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL FESTIVAL 2018

UBALOZI WA CHINA NCHINI WAMKABIDHI ZAWADI YA PIKIPIKI 10 MKURUGENZI WA TAASISI TA TULIA TRUST KWA AJILI YA WASHINDI WA TAMASHA LA TULIA TRADITIONAL FESTIVAL 2018

1 (13)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kutoka kwa Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya. (Picha na Muhidin Sufiani)

2 (14)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akisainiana hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozini hapo jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jini Mbeya. (Picha na Muhidin Sufiani)

3 (12)

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kwa ajili ya washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya. (Picha na Muhidin Sufiani)

Na Muhidin Sufiani
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust Dk.Tulia Akson, ameushukuru ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kuendelea kumdhamini katika Tamsha lake kwa kumkabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya washindi watakaopatikana kwenye tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 jijini Mbeya.Dk.Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekabidhiwa pikipiki hizo leo katika ubalozi huo na Mwakilishi wa Balozi wa China Tanzania nchini Xu Chen.
Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo Dk.Akson amesema anaushukuru ubalozi huo kwa kutoa zawadi hizo kwa ajili ya washindi 10 wa kwanza kutoka katika kila kundi katika tamasha hilo ambalo litafanyika kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 22 mkoani Mbeya.
“Kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust tunatoa shukrani zetu kwa ubalozi wa China nchini Tanzania kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi katika kusaidia zawadi kwa ajili ya washindi wa tamasha letu la Jadi la Tulia Traditional Festival 2018.
“Wadau wetu hawa mwaka jana pia walitoa pikipiki 10 ambazo tulikabidhi kwa washindi.Lengo la tamasha hili ni kukuza utamaduni wetu na hasa kwa kuanza na ngoma za asili lakini tunataka wanaoshiriki pia wanajikwamua kiuchumi,”amesema Dk.Akson.
 
 
 

About regina

Check Also

4-4

SERIKALI YAWAJAZA MAPESA BILIONI 688 WAKANDARASI WA MRADI WA UMEME WA RUFIJI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akimkabidhi Katibu Mkuu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − one =