Saturday , October 20 2018

Home / SIASA / BOMBOKO AMSHUKIA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE KAMA KIPANGA

BOMBOKO AMSHUKIA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE KAMA KIPANGA

IMG_0564

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umesema unaamini Juhudi anazofanya Rais John Magufuli ndani ya serikali yake ndio siri ya cha chama hicho kushinda kwenye uchaguzi wa marudio uliomalizika hivi karibuni.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar na Katibu wa chipukizi na uhamasishaji wa Umoja huo,Hassan Bomboko,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika  mkutano alipokuwa akijibu tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti Taifa wa chama cha  Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe kuwa CCM walishinda kutokana na wizi wa kura.

Bomboko amesema madai hayo sio ya kweli kwani chama hicho kimeshinda kutokana kile anachodai ni kasi ya utendaji wa Rais magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Amesema kwa sasa serikali ya Rais Magufuli imefanya mambo mengi mazuri ambayo yamewapendeza wananchi mpaka yakawafanya wachague wagombea wa Chama cha mapinduzi.

Ameongeza kuwa miradi mbali ya ujenzi wa Reli,Barabara,Madaraja Miundombinu ya Umeme pamoja kudhibiti rushwa, madwawa ya kulevya  na kuleta nidhamu katika utumishi wa Umma ni vitu pekee vinavyokipa nguvu chama hicho kuaminika kwa wananchi.

Amemtaka Mbowe kuacha visingizio na badala yake atafute sababu ya kushindwa kwa chama chake.

Hata hivyo,Mwanasiasa huyu amesema kama chama chochote hakiridhiki na matokeo hayo kifuate sheria ikiwemo kwenda kufungua kesi mahakamani .

About bukuku

Check Also

IMG_20181014_112001_199

HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI

 Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akimkabishi chetu mbunge mteuliwa wa Jimbo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − 15 =