Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAMLAKA ZA MAJI ZATAKIWA KUJIENDESHA KIBIASHARA

MAMLAKA ZA MAJI ZATAKIWA KUJIENDESHA KIBIASHARA

1

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla akimkaribisha Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili mkoani Katavi kukagua miradi ya maji.

2

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla wakiwa kwenye jengo la ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mzingira mjini Katavi (MUWASA), kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA, Mhandisi Zacharia Nyanda.

3

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwenye chanzo cha Ikolongo II kilichopo katika Wilaya ya Mpanda Vijijini, mkoani Katavi.

4

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akipokea maelezo katika eneo la chanzo cha Ilongo I kilichopo katika Wilaya ya Mpanda Vijijini, mkoani Katavi.

5

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Mpanda (MUWASA), Mhandisi Zacharia Nyandaa akitoa maelezo kuhusu mradi wa Ikolongo katika Wilaya ya Mpanda Vijijini, mkoani Rukwa.

……………………….

Mamlaka za Maji nchini zimetakiwa kujiendesha kibiashara kwa faida na kujitegemea katika shughuli zake za kila siku na kuacha kutegemea fedha kutoka wizarani.

Mamlaka hizo ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikitegemea ruzuku kutoka wizarani, zimetakiwa kujipanga vizuri kwa kuongeza mapato, kupanua mitandao wa maji na kuongeza wateja zaidi.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametoa rai hiyo wakati alipoanza ziara yake kikazi mkoani Katavi na kusisitiza chini ya uongozi wake mamlaka zijigharamie zenyewe gharama zake zote za uendeshaji.

Profesa Mbarawa amesema kwa muda mrefu mamlaka hizo zimekuwa kama idara za wizara hiyo kwa kutegemea kulipiwa umeme, utekelezaji wa miradi yake na gharama mbalimbali lakini jambo hilo hakubaliani nalo na lazima mamlaka hizo zijiendeshe kwa faida.

Lengo ni kuimarisha mamlaka zetu za maji na kuzijengea uwezo kwa lengo la kusimama na kujiendesha zenyewe kimkakati bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini. Kwa kufanya hivi zitatoa huduma bora na za uhakika kwa wateja wake; hili litapunguza changamoto na kero kwa wateja wake.

‘‘Tumetumia fedha nyingi sana kwa ujenzi wa miradi mikubwa Dar es Salaam, Morogoro, Musoma, Sumbawanga, Singida na maeneo mengine mengi mijini; huo ni mtaji tosha wanachotakiwa ni kuiendeleza. Serikali tumewekeza, wao wanatakiwa watumie fursa hiyo kujiendesha kibiashara na kuingiza faida’’, alisema Profesa Mbarawa.

‘‘Ongezeni makusanyo ya mapato na wigo wa wateja wenu, fanyeni upanuzi wa miradi na muongeze mitandao zaidi; kwa kufanya hivyo ni lazima mpate fedha za kutosha na kuacha kuitegemea wizara ambayo imejikita zaidi katika kuimarisha huduma ya maji vijijini. Ni lazima niwe mkweli kwenu chini ya uongozi wangu jambo hilo ni mwiko,’’ alionya Profesa Mbarawa.

Ameongeza kuwa wizara itatoa msaada kwa zile mamlaka zenye uhitaji mkubwa na itakuwa tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kujiendeleza zaidi na baadae kuzirudisha; asilimia 65 ya wananchi waishio vijijini wanapata majisafi na salama ukilinganisha na mijini ambapo ni asilimia 75, kwa sasa tumepanga kutumia fedha nyingi tulizonazo kuimarisha hali ya upatikanaji wa maji vijijini.

Vilevile, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutunza vyanzo vya maji ili miradi inayojengwa iwe yenye faida na endelevu.

Makalla amesema vyanzo hivyo ni muhimu kwa kuwa vinategemewa kuzalisha maji kwa ajili ya miradi inayojengwa, na kuwaasa wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo na kuwa walinzi wa vyanzo hivyo dhidi ya uchafuzi na uharibifu.

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × five =