Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / MGALU – TUSHIRIKIANE KUKABILIANA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA/TULINDE VYANZO VYA MAJI ILI KUFANIKISHA MRADI WA STIGLER’S GORGE

MGALU – TUSHIRIKIANE KUKABILIANA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA/TULINDE VYANZO VYA MAJI ILI KUFANIKISHA MRADI WA STIGLER’S GORGE

IMG-20180924-WA0011

Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa stigler’s gorge Rufiji. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

IMG-20180924-WA0010

Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa stigler’s gorge Rufiji, huku akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa CCM Pwani na wilaya hiyo. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

images_1537778837219

Sehemu ya eneo la maporomoko ya mto Rufiji mkoani Pwani. (picha na Mwamvua Mwinyi) 

NA MWAMVUA MWINYI,RUFIJI
WIZARA ya nishati imetoa rai kwa watendaji ,wadau na jamii kushirikiana ,kukabiliana na uhifadhi wa mazingira na kulinda vyanzo vya maji katika kutekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji -hydro power (Stigler’s Gorge).
Mradi huo ni mkubwa ambapo kipindi cha maandalizi ya kuanza mradi utatumika bilioni 700 ,na kwasasa hatua za mwisho za kumpata mkandarasi na msimamizi wake zinaendelea .
Hayo yalibainika wakati Naibu Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu ,alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati ya kitaifa Kibiti na Rufiji huku akiwa ameambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Pwani .
Alieleza ,kidakia maji hakina athari ila kuna tatizo la athari za kibinadamu ikiwemo kilimo katika vyanzo vya maji .
“UNESCO wamekubali hoja zao juu ya wazo la kufanikisha mradi huu ,kufuatia hatua hiyo ninaamini tukishirikiana kwa kuzungumza lugha moja ,tutatekeleza na kufanya kazi iliyokusudiwa ya kuweza kuzalisha umeme hapa megawatts 2,100 ” alisisitiza Subira.
Aidha alisema ,Kinyerezi I ,itaingiza megawatts 185 kwenye gridi ya Taifa, mwezi Desemba mwaka 2018.
Subira alifafanua ,umeme una faida kwa Taifa na mradi huo ni moja ya uzalishaji mkubwa wa umeme wa uhakika hapa nchini .
Alielezea ,katika mahitaji ya umeme ni suala muhimu ,ukizingatia kipindi hiki cha nchi inapoelekea kwenye uchumi wa kati na ongezeko la ujenzi wa viwanda hivyo haiwezekani kufikia malengo hayo kama hakuna umeme wa uhakika .
Hata hivyo ,alisema kuwa ,umeme unaozalishwa kwa gesi ni asilimia 49 ikiwa ni zaidi ya megawatts 1,500 .
Subira alielezea ,matarajio ni kuzalisha megawatts 5,000 ifikapo 2020 na mipango inaendelea zaidi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa umeme katika baadhi ya maeneo nchini .
Awali hydorogist mradi wa Stigler’s Gorge ,Stanslaus Kizzy alisema ,
bwawa hilo litawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika lakini pia nchi itatangazwa kwenye medani za Kimataifa .
Alisema ,bilioni 700 ni kwa ajili ya mwaka huu wa fedha kuandaa mradi kwani serikali imejipanga kila mwaka kati ya miezi 36 ya ujenzi kutenga fedha kufuatana na kazi itakavyokuwa .
“Kazi ya kwanza ni maandalizi kuchepusha mto ,pili itakuwa kujenga ukuta mwisho ni kujenga nyumba itakayowekwa mitambo Tisa ambayo kila mtambo mmoja utazalisha megawatts 235 sawa megawatts 2,115 ” alisema Kizzy .
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno alisema wamejionea hatua ilipofikia mradi ,na kusema utafungua milango ya kibiashara ,ajira ,uchumi na kuweka rekodi kidunia .
Maneno alisema ,wananchi wa vijiji jirani pia watanufaika moja kwa moja kuunganisha na kupata umeme wa uhakika .

About regina

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty − ten =