Thursday , December 13 2018

Home / MCHANGANYIKO / MWANAFUNZI MBARONI KWA KUTUPA KICHANGA CHOONI

MWANAFUNZI MBARONI KWA KUTUPA KICHANGA CHOONI

MATEI

Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo, Ines Mtundu (19) anamshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga baada ya kujifungua.

Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Mate wakati akizungumza na wanahabari.

“Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo,” amesema Kamanda Matei.

Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, Kamanda Matei amesema mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto mchanga akiwa hai.

“Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani,” ianeleza sehemu ya taarifa hiyo.

About regina

Check Also

????????????????????????????????????

Wafanyakazi wa TBL Mbeya na Arusha wapatiwa elimu ya kupinga Ukatili wa kijinsia

Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL)  mwaka huu kwa mara nyingine imeungana na mashirika yanayopinga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

4 × 5 =