Thursday , December 13 2018

Home / MCHANGANYIKO / MWASELELA AWASAIDIA WAJANE USHARIKA WA KKKT FOREST MBEYA

MWASELELA AWASAIDIA WAJANE USHARIKA WA KKKT FOREST MBEYA

 

 

 Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela akizungumza wakati wa Ibada katika kanisa la KKKT Forest Mbeya juu ya umuhimu wa utoaji kwa jamii.

 Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela, akikabidhi fedha kwa wajane ambao aliomba wasaidie katikati ya ibada

Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela  akiombewa na Mchungaji  Kiongozi wa Usharika wa KKKT Forest Mbeya.


Mkurugenzi wa Shule za Patrick Mission na Mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela  akiagana na Mchungaji wa Usharika.

Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii Mbeya

Mkurugenzi
wa Shule za Patrick Mission na mdau wa Maendeleo Ndele Mwaselela atoa msaada
kwa wajane wawili katika kanisa la KKKT Forest Mkoani Mbeya .

Mwaselela
ambaye alipata nafasi ya kuzungumza na wanakwaya wa kwaya ya Safina ya kanisa
hilo ambapo aliomba apewe wajane wawili hili aweze kuwapatia mitaji hili waweze
kujikwamua kimaisha.

“Mimi ni
Mtoto wa Mama ntilie ambaye nimefanikiwa leo hivyo niwaambie wazi Mama yangu
alikuwa anauza Supu hili mimi nisome hivyo ninakilasababu  ya wajane hivyo naona fahari kila ninapofika
mahali niweze kuwagusa wanawake wawili” amesema Mwaselela.

Mwaselela
amesema kuwa mbali ya kuwa mtoto wa Mama Ntilie walitokea watu wakainuka
wakanisomesha na wengine sasa ni wabunge na wamepata kushika nafasi za Juu
serikalini.

Amesema kuwa
ni vyema watu wakajifunza kutoa na kusaidia wengine kwani kwa kufanya hivyo
Mungu ugusa pale walipotoa na kuwabariki kwa kila hatua wanayopita.

Mwaselela
alimaliza kwa kusema ni vyema jamii ya Watanzania iweze kujifunza namna ya
kusaidia wengine kwa kile kidogo wanachokipata katika shughuli zao za kila
siku.

About regina

Check Also

GY3A9651

Mahiga:Tuadhimishe Uhuru kwa kuwakumbuka waliopigania Uhuru huo

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen − nine =