Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / DC PANGANI AGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MAUAJI YA BODABODA WILAYANI PANGANI

DC PANGANI AGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MAUAJI YA BODABODA WILAYANI PANGANI


 

MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah (kulia)
akimfariji mama wa dereva wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally
alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa
alikodisha na watu wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
 

MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah (kushoto) akimpa
pole mama wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally alimaarufu Sharo
anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa alikodisha na
watu
wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
 

MKUU wa wilaya ya Pangani
Zainabu Abdallah (katikati) akiteta jambo na ndugu wa marehemu kushoto
ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Nyange Hassani katikati
ni Afisa Tawala wa wilaya hiyo Gipson

 MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani
Tanga Zainabu Abdallah ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani
humo kufanya uchunguzi wa kina ufanyike ili kuweza kubainika sababu za
mauaji ya dereva wa bodaboda Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya
kazi zake Pangani mjini.

Inadaiwa mauaji ya bodaboda huyo yalitokea jioni ya Septemba 22 mwaka
hu na mwili wake kupatikana Jumapili na kuzikwa juzi mara baada ya
kukodiwa na watu wasiojulikana ambao walitaka awapeleka Tanga mjini na
walipofika njiani wakatekeleza mauaji hayo kwa kumnyonga hadi umauti
ulipomkuta na kuchukua pikipiki yake kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza mara baada ya kuitembelea familia ya marehemu na
kutoa pole, Mkuu huyo wa wilaya alisema wamepokea kwa masikitiko
makubwa na mshtuko wizi huo na mauaji hayo ya bodaboda ambaye ni
kijana mjasiriamali.

“Kijana huyui mkazi wa Pangani ameuwawa kikatili sana kwa kunyongwa na
watu wasiokuwa na utu na kuchukua pikipiki aliokuwa akifanyia biashara
….inaumiza kijana asie na hatia anayejitafutia riziki kujikwamua
kimaisha ndoto zake zinakwamishwa”Alisema.

Aidha alisema wanalaani vikali vitendo hivyo huku akiviagiza vyombo
husika kufanya uchunguzi wa tukio hilo haraka ili wahusika waweze
kuchukuliwa hatua kwa kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria.

Hata hiyo alisema wanatarajia kukutana na kuongea na chama cha
waendesha BodaBoda wilaya ya humo kuhusu jambo hili na mustakabali wao
hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

About regina

Check Also

DSC_1529

UJUMBE WA WATU 11 KUTOKA OMAN WAFANYAZIARA MAALUM ZANZIBAR

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fifteen − 9 =