Thursday , February 21 2019

Home / MICHEZO / LUKA MODRIC MWANASOKA BORA WA DUNIA WA FIFA 2018

LUKA MODRIC MWANASOKA BORA WA DUNIA WA FIFA 2018

Luka Modric amemaliza utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo za Wachezaji Bora binafsi duniani.

 

WASHINDI WOTE WA TUZO ZA FIFA 2018: 

Tuzo ya Puskas
4522388-6203061-image-a-32_1537816973541
Mohamed Salah
Kocha Bora wa Kiume wa Mwaka 

4522250-6203061-image-a-19_1537816199777-950x650

Didier Deschamps
Kocha Bora Kike wa Mwaka
Reynald Pedros 
Kipa Bora wa Mwaka
4522492-6203061-image-a-35_1537817633203-950x845
Thibaut Courtois 
Mwanasoka Bora wa Kike 
4523228-6203061-image-a-71_1537820134262-950x670
Marta
Tuzo ya Mwanasoka  Bora wa Kiume wa Mwaka wa FIFA
4522988-6203061-image-a-49_1537819300264-950x633
Luka Modric
Kikis Bora cha FIFA FIFPro
4522978-6203061-image-a-60_1537819461991-950x602
David De Gea; Dani Alves, Raphael Varane, Sergio Ramos, Marcelo; Luka Modric, N’Golo Kante, Eden Hazard; Lionel Messi, Kylian Mbappe, Cristiano Ronaldo.
 

KIUNGO Luka Modric amemaliza zama za utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo za Wachezaji Bora binafsi duniani.
Hiyo ni baada ya Modric kuwazidi wapinzani wake, Ronaldo na Mohamed Salah wa Liverpool na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kiume wa Mwaka wa FIFA katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Royal Festival mjini London.
Na hiyo ni baada ya Modric kufanya vizuri katika klabu yake, Real Madrid mwaka 2018 akiiwezesha kushinda mataji ya Ligi ya Mabingwa kabla ya kuiongoza timu yake ya taifa, Croatia kufika fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi ambako ilifungwa na Ufaransa. 
“Ni heshima kubwa na hisia nzuri kusimama hapa na taji hii maridadi,” Modric said.
“Kwanza kabisa ningependa kuwapongeza Mohamed na Cristiano kwa msimu mzuri waliokuwa nao.
“Taji hili si la kwangu tu, ni la wachezaji wenzangu pia wa Real Madrid, la wachezaji wenzangu wote wa timu ya taifa ya Croatia, ya makocha wote niliocheza timu zao. Bila wao, hili lisingewezakana,”. 
Kisha Modric akamgeukia kiungo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Misri, Salah, aliyehudhuria tuzo hizo huku nyota mkubwa wa Juventus, Ronaldo akibaki Italia.
“Nina uhakika siku zijazo utapata nafasi nyingine ya kupigania tuzo hii,”alimalizia.
Mchezaji mwenzake Modric, Gareth Bale amempogeza kwa ushindi huyo kupitia akaunti yake ya Instagram:?
Nyota wa zamani, Mbrazil Brazil Pele pia amempongeza Modric kwa ushindi huo.

About Alex

Check Also

Yangarahapic

YANGA SC YAVUNJA MWIKO CCM KIRUMBA MWANZA, YAICHAPA 2-1 MBAO FC

Na Mwandishi Wetu, MWANZA YANGA SC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Mbao FC …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen + 3 =