Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / MABULA AWATULIZA WANANCHI KIJIJI CHA SOGA MKOA WA PWANI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI DHIDI YA MUWEKEZAJI

MABULA AWATULIZA WANANCHI KIJIJI CHA SOGA MKOA WA PWANI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI DHIDI YA MUWEKEZAJI

01

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Soga Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani wakati alipokuenda kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

03 (1)

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akitoa maelekezo wakati akikaangalia ramani ya mashamba eneo la Soga Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani wakati alipokuenda kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

04 (2)

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akioneshwa sehemu ya eneo la Soga Halmashauri ya Wilaya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani na Mpima Ardhi kutoka Wizarani Idrisa Mwaikasa (wa pili kushoto) wakati alipokuenda kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

05 (1)

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia mbolea aliyoiona wakati wa ziara yake ya kutatua migogoro ya ardhi katika mkoa wa Pawani jana, kulia ni Mpima Ardhi wa Wizara Idrisa Mwaikasa.

02

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Soga Halmashauri ya Wilaya Kabaha Vijijini mkoa wa Pwani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alipokuenda kusikiliza mgogoro wa ardhi eneo hilo.( Picha zote na Munir Shemweta)

Na Munir Shemweta, Kibaha

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewataka wananchi wa kijiji cha Soga Wilaya ya Kibaha vijijini mkoa wa Pwani kuishi kwa amani katika eneo hilo  wakati serikali ikishughulikia mgogoro baina yao na mwekezaji kampuni ya Mohamed Enterprises.

Mabula alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara katika kijiji hicho kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa ardhi baina ya wananchi wa kijiji hicho na kampuni ya Mohamed Enterprises inayomiliki eneo kubwa katika kijiji hicho jambo linalowatia hofu wananchi kuondolewa katika eneo hilo.

Aliwaambia wakazi wa kijiji hicho kuwa lengo la ziara yake ni kujionea hali halisi ya eneo kwa kuwa ni vigumu kutatua mgogoro bila kufika katika eneo la tukio.

Alisema, serikali imesikia kilio cha wananchi hao ambao wapo tangu mwaka 1975 na serikali haiwezi kuwafukuza kwa kuwa iko kwa ajili yao.

Kwa mujibu wa Mabula, Serikali inachoangalia sasa kama muwekezaji ameshindwa kuendeleza eneo alilomilikishwa kulingana na masharti basi umiliki utafutwa na katika ngogoro wa eneo hilo  tayari Afisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijni amepeleka  mapendekezo ya kufuta sehemu ya umiliki wa shamba hilo kutokana na ukiukwaji  masharti ya uwekezaji.

‘’Kinachosubiriwa sasa ni mchakato mzima na suala hilo na tayari lishapelekwa kwa mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua za utekelezaji’’ alisema Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mabula alimuagiza mkuu wa Wilaya ya Kibaha Asupta Mshana kuhakikisha hakuna mwananchi yoyote anayenyanyaswa kuhusiana na mgogoro huo na kusisitiza watakaofanya hivyo basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Awali wananchi wa kijiji hicho walitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa wamekuwa wakinyanayswa na muwekezaji kwa madai ya kuvamia eneo lake wakati wao walikuwemo tangu mwaka 1975.

Mkazi wa kijiji hicho Joseph Masana alisema, wananchi wa eneo hilo hawakatai uwekezaji  bali wanahitaji uwekezaji shirikishi ambapo muwekezaji atakuwa aenaendeleza mashamba badala ya kuyaweka kuwa mapori.

Alisema, wanachohitaji ni majadiliano na serikali kuhusu muwekezaji ambaye ameyaacha mashamba kuwa mapori bila ya kuyaendeleza.

About regina

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − 19 =