Thursday , December 13 2018

Home / filamu / TANZANIA YATHIBITISHA KUANDAA MICHUANO YA FAINALI ZA VIJANA

TANZANIA YATHIBITISHA KUANDAA MICHUANO YA FAINALI ZA VIJANA

index
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)imeithibitisha rasmi Tanzania kuwa wenyeji wa Fainali za Africa za Vijana zitakazofanyika mwakani.
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kimekutana kwa siku mbili huko Sharm El Sheikh,Misri. 
Kupitia sauti ya Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,Serikali ya Tanzania ilimthibitishia Rais wa CAF Ahmad Ahmad utayari wa kuwa wenyeji wa mashindano hayo na kwamba tupo tayari kufanya juhudi kubwa za maandalizi.
Shindano hilo litafanyika kuanzia April 14 mpaka April 28, 2019. 
Timu zilizofuzu kucheza fainali hizo ni Angola, Cameroon, Guinea, Morocco, Nigeria, Uganda, Senegal na wenyeji Tanzania. 
Droo kwaajili ya mashindano hayo itafanyika Desemba 20 nchini Tanzania. 
Wakati wa michezo ya kufuzu kucheza fainali hizo nchini Tanzania UEFA walihusika katika upande wa fedha na ufundi ambapo wataalamu wa ufundi wa UEFA walishirikiana kwa karibu na wale wa CAF. 
Zoezi la kupima umri(MRI) katika michezo hiyo ya kufuzu imefanya shindano hilo kuwa na thamani zaidi.

About bukuku

Check Also

4-2

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI ATOA SALAMU ZA KUMBUKUMBU YA MIAKA 57 YA UHURU WA TANZANIA BARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa Salamu za miaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 + 9 =