Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / LIONS CLUB YATOA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO KWA WATOTO 486 MKOANI ARUSHA

LIONS CLUB YATOA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO KWA WATOTO 486 MKOANI ARUSHA

Rotary Medical Camp-62

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Watoto mia nne na themanini na sita kutoka shule mbalimbali za msingi wamefanyiwa vipimo vya macho ambapo wawili katai yao wakibainika macho yao kuharibika kabisa na kusababisha upofu hali inayowalazimu kupelekwa shule maalum ambapo wanane wakipewa rufaa kwenda hospitali ya KCMC kwa ajili ya upasuaji mkubwa.

Akizungumza wakati wakiendesha zoezi hilo la upimaji katika shule ya msingi Meru jijini hapa zoezi lililoendeshwa na klabu ya Lions kiongozi wa klabu hiyo Chifu Maswanya amesema kuwa zoezi hilo  lengo lake ni kuwafikia watoto elfu moja wa shule mbali mbali jijini hapa.

Amesema kuwa zoezi hilo la uoni hafifu kwa watoto linatajwa kuwa moja ya changamoto kubwa ya wanafunzi kufikia maengo yao katika kupata elimu na upokeaji duni inayotolea shuleni.

“Taasisi yetu imeona jambo hili la uoni hafifu linawanyiama watoto wetu kufikia malengo ya maendeleo yao shuleni hivyo tukaona tuendeshe zoezi hili kusaidia maendeleo yao”alisema Maswanya.

Kwa Upande wake mwakilishi wa elimu msingi kutoka halmashauri ya jiji la Arusha Denis Kanana alisema kuwa Anaishukuru Taasisi ya Lions Club ya mkoani Arusha kwa zoezi hilo ambalo litasaidia kukuza taaluma mashuleni kwa watoto kupokea masomo vizuri na hivyo ufaulu kupanda.

Amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha watoto wengi wanafikiwa na huduma hiyo ili kuondoa changamoto ya kutoona inayowapunguzia uelewa mzuri wa masomo kwa kushindwa kuona au kusikia kwa ukaribu.

“Natoa rai kwa taasisi mbali mbali kuisaidia serikali kuweza kuwapatia huduma muhimu zitakazowasaidia vijana wetu kutimiza malengo yao sanjari na ndoto zao za kielimu na kitaaluma ili waweze kuja kuisaidia nchi wakati ujao”alisema Kanana

Nae Mratibu wa Afya ya macho wa jiji la Arusha Glory Ndossi amesema hadi sasa zoezi hilo limewafikia watoto mia tatu na ishirini na nane ambao wamebainika kuathiriwa na mzio na kupatiwa dawa na wengine kumi na wane wakisubiria upasuaji wa kawaida.

Amesema kuwa pamoja na zoezi hilo kwenda vizuri watajitahidi kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu ili kuweza kupambana na maradhi hayo mapema kwa vijana wetu kuondoa athari kubwa hapo baadae.

“Tumetoa huduma ya upimaji kwa vijana wetu hawa wa shule za msingi hapa jijini na umeenda vizuri kwa vijana kupata vipimo na wengine dawa na wengine wanangojea kupata upasuaji katika sehemu mbali mbali”alisema Ndossi.

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eight + three =