Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / MBARAWA ASUBIRI MAJI KWA SAA MBILI NA NUSU

MBARAWA ASUBIRI MAJI KWA SAA MBILI NA NUSU

WhatsApp Image 2018-07-20 at 15.58.36

Na Ahmed Mahmoud ,ARUSHA
WAZIRI wa  Maji na Umwagiliaji Prof.Makame Mbarawa amelazimika kupiga kambi katika kijiji cha Levolosi Kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru kwa masaa mawili na nusu akisubiri kisima kinachochimbwa kitoe maji kabla ya kwenda kusaini mkataba.

Aidha amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumrudisha Wizarani mara moja Mhandisi  wa Miamba Amir Msangi  kwa uzembe wa kutoonekana kwenye eneo la mradi.

Waziri Mbarawa alitoa agizo hilo  jana wakati alipotembelea Kijiji cha Levolosi, Kata ya Kimnyaki kujionea zoezi la uchimbaji wa visima vitatu na baada ya hapo alitia saini ya mkataba wa ujenzi wa mtandao mpya wa maji,mitambo ya kutibu maji safi ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA na ujenzi wa ofisi kuu ya AUWSA Kanda ya Kati wenye thamani ya Sh.bilioni  520.

Prof.Mbarawa alisema serikali imeamua kuleta wataalam wake toka Wizarani ili wasimamie na kujifunza Teknolojia mpya ya uchimbaji visima vikubwa kwa ajili ya kuweza kufundiaha wenzao utaalam huo hapo baadaye.

“Lakini cha kushangaza nimepata taarifa huyu Amir Msangi haonekani dneo la kazi na hivyo namwagiza mtaalam mwenzake Fatuma Mambo kumtaarifu Katibu Mkuu ili arudishwe Wizarani huyu na hapa aletwe mwingine atakayepata ujuzi huu,”alisema

Alisema lengo pia la serikali kuwaleta wataalam hao ili kuhakikisha miradi ya maji inayotekelezwa inakuwa na ubora uliokusudiwa.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi kupata maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.

Aidha alisema miradi hiyo inatekelezwa na AUWSA kwa ufadhili wa serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruth Koya alisema mradi huo utakamilika  Juni mwaka 2020 na wanatarajia Arusha itanufaika na mradi huo kwa kuwa ukosefu wamaji utakua historia.

“Kwa kuanza tayari wakandarasi wameanza kusambaza mabomba ya maji taka nakuweka ya kisasa namakubwa yanayoendana na mahitaji ya sasa,lengo mazingira yawe safi na wananchi wapate huduma zamaji safi bila shida,”alisema
Alisema zaidi ya wananchi 827,000 watanufaika na mradi huo ambao utazalisha maji lita milioni 200 kwa siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya AUWSA, Dk.Richard Masika alisema ili miradi hiyo inayotekelezwa sasa  iwe mfano na endelevu wamewapatia mafunzo Timu ya Menejimenti na watumishi wengine toka kwa wataalamu wa Jumuiya  ya kusimamia mikataba ya Kimataita.
“Ili kukwepa gharama serikali tulimgharamia kuleta wataalam hawa toka nchi ya Switheland.

About Alex

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × four =