Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI YAWATAKA WADAU KUWEKEZA KWENYE UTALII WA UTAMADUNI

SERIKALI YAWATAKA WADAU KUWEKEZA KWENYE UTALII WA UTAMADUNI

DSC04911

Na Ahmed Mahmoud Arusha
SERIKALI imewaomba wadau wa Utalii nchini kuwekeza kwenye utalii  wa Utamaduni na wa kiasili kwa kuwa ni kivutio kikubwa cha utalii wa kawaida.

Rai hiyo imetolewa Oktoba 9 na Katibu mkuu wizara ya Habar, Utamaduni na Michezo, Suzan Mlawi ,alipokuwa akizindua rasi tamasha la Urithi wa asili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha.

Amesema kuwa moja wapo ya lengo la tamnasha hilo ni kuibua vipaji  na kuhifadhi  na kurithisha urithi huo na  kutokana na uwekezaji kwenya utalii wa utamaduni na kiasili  kutaongeza pato linalotokana na utalii
.
Awali  Mkurugenzi  mkuu wa Makumbusho ya taifa Profesa Audax Mabura,amesema Tanzania ina urithi  mkubwa pia urithi mwingine haujulikani ambao ni wa utamaduni.

Mabura,ambae pia ni mwenyekiti wa tamasha hilo amesema urithi wa utamaduni ambao  sio hai  unahusisha masalia ya viumbe vya kale ikiwemo watu wa kale ulimwenguni,yaani Zamadamu, walioishi miaka milioni 2 iliyopita ambao walifanikiwa kutengeneza  zana za maewe na utamaduni ulianzia hapo

Amesema pia upo urithi mwingine wa michoro  kwenye miamba ya mawe ambao unatambuliwa na shirika la umoja wa mataifa la Sayansi na Elimu,Unesco  kwa kipindi cha miaka 40 sasa na hivyo kuifanya Tanzania kutambulika kama chimbuko la biadamu duniani.

Profesa Mabura,amesema tamasha hilo lenya kauli mbiu isemayo, Urithi wetu fahari yetu, lina malengo mawili la kwanza ni kuendeleza,kutambua,kuhifadhi na kurithisha kizazi kijacho. na lingune lengo  ni kuendeleza urithi  uwe ni zao la utalii.

Amesema tamasha hilo lilizinduliwa rasmi mkoani Dododma Septemba 15 mwaka huu na Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan, na kuhudhuriwa na wananchi 7500 kwa muda wa wiki nzima na baada ya hapo limezinduliwa Zanziba, Dar es salaam,lilikuwa lizinduliwe Mwanza lakini kutokana na ajali ya Kivuko cha MV Nyerere wameahirisha uzinduzi utafanyika mwakani.

Profesa Mabura,amesema kwenye uzinduzi huo makamu wa rais aliiagiza mikoa yote nchini kutenga bajeti ya  kuendeleza tamasha hilo la urithi liwe linafanyika kila mwaka .

Kwa upande wake mkurugenzi wa Mamlaka ya wanyama pori,TAWA, James Wakibara,akitoa salamu za wizara hiyo amesema wizara ya Maliasli na Utalii ilibuni  tukio la kuwepo urithi wa kuenzi milaa , desturi na tamaduni zetu  kwa kuchelewa .

Amesema licha ya kuchelewa kulizindua tamasha hilo linalenga kuzienzi ,Kwa kudumisha urithi  wetu  bado watalii hawajalitambua tukio hilo ili likikomaa litakuwa na ongezeko la watalii hivyo kuongeza pato linalotokana na utalii.

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − four =