Tuesday , March 26 2019

Home / BIASHARA / TBL YATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA MWAJIRI BORA NCHINI TENA!

TBL YATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA MWAJIRI BORA NCHINI TENA!

TOP PHOTO 2
Meneja wa ukuzaji vipaji vya TBL,Lilian Makau akifurahia ushindi
TOP PHOTO 3
Meneja wa Ukuzaji Vipaji wa TBL,Lilian Makau akifurahia tuzo hiyo wakati wa hafla iliyofanyika nchini Afrika ya Kusini
TOP PHOTO 4
Nembo maalum ya tuzo hiyo
TOP PHOTO
Kikombe cha Tuzo ya Mwajiri bora kilichotolewa na taasisi ya Top Employers Institute kwa kampuni ya  TBL
………………………
Taasisi ya kimataifa ya masuala ya Raslimali Watu na ajira ijulikanayo kama Top Employer Institute yenye Makao yake makuu nchini Uholanzi imeitunukia tuzo ya Mwajiri Bora 2018 kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), kutokana na kuzingatia na kutekeleza kanuni za Raslimali Watu na uajiri ipasavyo ikiwa ni ushindi wa mwaka wa pili mfululizo ambapo mwaka jana pia ilishinda tuzo hiyo.
Vigezo vya ushindi vimetokana na utafiti wa taasisi ya Top Employers kwa makampuni mbalimbali makubwa nchini ambao ulilenga kwenye  utekelezaji kanuni za ajira na Raslimali watu,  kampuni ya TBL imebainika kuwa na vigezo vya  ubora katika utekelezaji wa kanuni za ajira zinavyotakiwa.
Baadhi ya vigezo ambavyo vilifuatiliwa katika utafiti huo kutoka kwa waajiri ni mikakati ya kukuza vipaji vya wafanyakazi,mpangilio wa kazi wa kila siku,mazingira ya kazi,uendelezaji wafanyakazi kimafunzo,utawala sehemu za kazi,taaluma na upandishaji wa vyeo kwa wafanyakazi,maslahi ya wafanyakazi na malipo ya stahiki zao kwa ujumla na desturi ya kampuni.
Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa TBL,David Magese alisema “Kampuni yetu inajivunia kupata  tuzo hii kwa kipindi cha miaka 2 mfululizo,hii inadhihirisha mwendelezo wa  dhamira yetu wa kuifanya kampuni yetu mwajiri bora anayekidhi viwango vya ndani na vya kimataifa,”
Magese aliongeza kusema kuwa TBL mbali na kushinda tuzo hii ya uajiri bora ngazi ya kimataifa pia inashikilia rekodi ya kuwa mwajiri bora nchini ambapo mwaka 2015 na 2016 ilishinda tuzo ya Mwajiri Bora inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).“Tunajivunia kwa mafanikio ya kampuni inayoendelea kuyapata na tutazidi kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wetu kwa kuwa ni moja ya sera yetu”.Alisema Magese.
Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Top Employers Institute,David Plink,alisema tuzo ya Mwajiri Bora imetolewa kwa  TBL kutokana na kuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wake sambamba na uekelezaji wa kanuni za ajira zinazojali wafanyakazi  na kutangazwa kuwa  kampuni bora  inayoongoza katika masuala ya ajira kwa kipindi cha mwaka huu baada ya kuibuka tena mshindi mwaka uliopita.
TBL ilitangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo hii katika hafla iliyofanyika Johanesburg nchini Afrika ya Kusini.

About Alex

Check Also

image1

BOOMPLAY KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA WARNER MUSIC GROUP

DAR ES SALAAM, TANZANIA Boomplay ni app inayotoa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − 7 =