Tuesday , December 11 2018

Home / MICHEZO / TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND ZAANZA KUMSAKA MBWANA SAMATTA

TIMU ZA LIGI KUU ENGLAND ZAANZA KUMSAKA MBWANA SAMATTA

43433437_328824004561357_5369003492763500544_n

Nyota ya Mtanzania, Mbwana Ally Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk huko Ubelgiji imezidi kung’aa baada ya kuanza kuwaniwa na vilabu vikubwa barani Ulaya.

Taarifa ambazo zipo mitandaoni hivi sasa kutoka vyanzo kadhaa huko England zinaeleza kuwa nyota huyo anawaniwa na klabu tatu zinashoriki ligi kuu England.

West Ham, Everton na Burnely zimetajwa kuanza kumvutia waya Samatta ambaye amekuwa tegemeo ndani ya klabu yake.

Samatta ameingia kwenye vichwa vya habari England ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu aanze kuhusishwa kutimkia Spain katika timu baadhi zinazoshiriki Ligi Kuu ‘La Liga’

Mchezaji huyo hivi sasa yupo hapa nchini tayari kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kuelekea AFCON 2019 na kikosi cha Taifa Stars.

About Alex

Check Also

7212630-6477327-image-m-19_1544394932492

RIVER PLATE WAIPIGA BOCA JUNIORS NA KUBEBA COPA LIBERTADORES

Wachezaji wa River Plate wakifurahia na taji lao la Copa Libertadores baada ya ushindi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 − one =