Thursday , February 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / MBUNGE COSATO CHUMI ABANWA NA WANANCHI TATIZO LA UMEME KATIKA KIJIJI CHA RUNGEMBA

MBUNGE COSATO CHUMI ABANWA NA WANANCHI TATIZO LA UMEME KATIKA KIJIJI CHA RUNGEMBA

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akitolea ufafanuzi juu ya swala la tatizo la umeme mara baada ya kupigia simu meneja wa tanesco wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
 
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Wananchi
wa kata ya Rungemba mkoani Iringa wamemuweka kikaangoni mbunge wa jimbo la
Mafinga mjini Cosato Chumi juu ya kukosekana kwa umeme katika baadhi ya
vitongiji ya kata hiyo.
 
Wakizungumza
kwenye mkutano wa hadhara wananchio hao wamesema kuwa wamekuwa walinzi wa umeme
ambao umepita katika kijiji cha Rungemba.
 
“Sisi
watu wa Makwawa na Njia Panda tumekuwa walinzi wa huu umeme ambao umepita
kwenye hiki kijiji cha Rungemba na kata kwa ujumla maana hakuna hata laini ndogo
ambayo inasemekana imepita lakini tumekuwa tunashangaa maana hakuna hata hiyo laini”
walisema wananchi hao
 
Wananchi
hao wameendelea kwa kusema kuwa umeme huo toka umefika hauna faida kwa wananchi
wa kijiji hicho kwa kuwa wamepelekewa transifoma yenye nguvu ndogo kulingana na
mahitaji ya wananchi.
 
“Tumewekewa
transifoma haina uwezo kwa kuwa inashindwa hata kusukuma mashine za kusagia
mahindi hivyo inatulazimu kusafiri zaidi ya kilometa saba kwa bodaboda kupata
huduma ya kusaga mahindi” alisema wananchi
 
Aidha
wananchi hao wamesema kuwa wapo tayari kulipia nguzo za umeme ili waweze kupata
nishati hiyo kwa maendeleo ya wananchi na kijiji hicho.
 
Naye
mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akaamua kumpigia simu meneja wa
tanesco wilaya ya Mufindi Omary Ally kupata ufumbuzi wa tatizo hilo mbele ya
wananchi.
“Meneja
nimebanwa hapa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi juu ya tatizo la umeme
hapa Rungemba hali ipoje” aliuliza swali kwa meneja?
 
Akijibu
hoja hizo meneja wa Tanesco wilaya ya Mufindi Omary Ally kuwa kulikuwa
kunatatizo la transifoma hiyo baada ya wiki moja watafunga na wananchi watapata
nishati ya umeme ya uhakika kabisa
 
Hata
hivyo Ally akawatoa hofu wananchi kwa kuwaahidi kuletea transiafoma ambayo
itakidhi mahitaji ya wananchi wa kijiji hicho na kuondokana na kero hiyo ambayo
inarudisha nyuma maendeleo.
 
Hatua
hiyo imekuja mara baada ya wananchi kata ya Rungemba kukaa kwa kipindi cha muda
mrefu bila kuwa na huduma hiyo ya umeme.
 
 

About Alex

Check Also

3

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 30

Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile akizungumza na wajumbe wa kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten + 18 =