Wednesday , April 24 2019

Home / MCHANGANYIKO / MRADI WA HAKI YETU WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA DOLA KIGOMA KUHUSU ULINZI WA WATU WENYE UALBINO

MRADI WA HAKI YETU WAZUNGUMZA NA VYOMBO VYA DOLA KIGOMA KUHUSU ULINZI WA WATU WENYE UALBINO

Baadhi
ya watendaji kutoka idara za Mahakama, Polisi na viongozi wa vijiji,
kata na mitaa kwenye halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma wahimiza
umuhimu wa kuimarisha ulinzi ili kupunguza madhila kwa watu wenye
ualbino, sambamba na kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na masuala ya
ualbino ili kuondoa dhana potofu, dhidi ya watu wenye ualbino ambayo
imejangeka miongoni mwa baadhi ya wananchi.

 
Pia jamii
kukumbushwa kuhusiana na maadili mema, sambamba na kuhakikisha
watendaji hao wanazingatia maadili yao ya kazi katika kuwahudumia
wananchi.
 
Maazimio hayo yamefikiwa baada ya
watendaji hao kupatiwa elimu kuhusu ualbino, maadili na amani,
iliyotolewa na mashirika ya CEFA Tanzania, GNRC Tanzania na Under The
Same Sun, ambayo kwa pamoja yanatekeleza mradi wa Haki Yetu.

 John Richard, Afisa Mawasiliano wa Mradi wa Haki Yetu,
akizungumza na baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka idara ya
Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu, mkoani Kigoma
kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Haki Yetu.

 

 Faustine Gwassa, Naibu Meneja wa Mradi wa Haki Yetu akichokoza
mada wakati wa mafunzo kwa baadhi ya watendaji wa kata, maafisa kutoka
idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya mji Kasulu,mkoani
Kigoma. 
Joyce Mdachi, kutoka shirika la
GNRC akifundisha umuhimu wa maadili na amani kwa baadhi ya watendaji
kata, maafisa kutoka idara ya Mahakama na Polisi kwenye halmashauri ya
mji Kasulu, mkoai Kigoma.

About Alex

Check Also

4-4

SERIKALI YAWAJAZA MAPESA BILIONI 688 WAKANDARASI WA MRADI WA UMEME WA RUFIJI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akimkabidhi Katibu Mkuu wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten + nineteen =