Friday , November 16 2018

Home / BURUDANI / UZINDUZI WA MSIMU MPYA WA VICHEKESHO VYA MWANTUMU

UZINDUZI WA MSIMU MPYA WA VICHEKESHO VYA MWANTUMU

1

Mkuu wa Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Alpha Mria akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa vichekesho vya Mwantumu iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya MultiChoice Tanzania.

2

Mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kama Joti  akizungumza wakati wa uzinduzi.  Joti amebeba uhuska wa  aina tatu tofauti katika vichekesho hivi ambapo anafahamika kama kijana Kaboba, kama binti Mwantumu Sahare na Mzee Mrisho,

3

Baadhi ya wageni waliohudhuria  katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa vichekesho vya Mwantumu katika ofisi za MultiChoice Tanzania.

………………..

Vichekesho vya Mwantumu vyaongezwa Udambwi-dambwi

·          Msimu wa pili waja kwa kishindo

·         Sasa kuonekana mara mbili kwa wiki

Msimu mpya wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo huonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo unaanza rasmi JumanneOktoba 16,  huku vikiwa vimeongezewa manjonjo ili kuwahakikishia watazamaji na mashabiki wake burudani isiyo na upinzani.

 

Vichekesho hivyo vinavyoongozwa na mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la kisanii JOTI ambaye kwenye vichekesho hiviamevaa uhusika wa watu watatu tofauti ; Mzee Mrisho, Kaboba na Mwantumu Sahare,  vimekuwa ni moja wa vipindi vinavyotazamwa sana nakupendwa na maelfu ya watu hapa nchini ambapo huonyeshwa kupitia chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Majina maarufu pia katikatasnia ya uigizaji na uchekeshaji yatakuwepo msimu huu akiwemo Mzee Fungafunga (Mzee Mwalubadu), Mama Abduli (Mwantumu Mcharuko), AlexWasponga(Kayombo) na wengineo wengi

 

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho hivyo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwatangu kuanza kwa msimu wa kwanza wa vichekesho vya Mwantumu mnamo Oktoba 2017, vichekesho hivyo vimekuwa na msisimko wa aina yake navimepokelewa vizuri sana na watazamaji na hivyo kuvifanya kuwa na mashabiki wengi sana.

 

Amesema msimu huu wa pili watazamaji wa Maisha magic Bongo na mashabiki wa Mwantumu watashuhudia mikasa ya aina yake ambapo baada ya Bahati kupata ujauzito, baba yake mzee Mwalubadu anaamua kumpeleka Kaboba katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumpa Bahati ujauzito. Hatahivyo suala hilo linafika kwa Babu yake Kaboba mzee Mrisho, ambaye wakati huohuo hataki Kaboba apate matatizo yoyote. Kinachotokea hapo nidrama ya aina yake itakayowaacha watanzamaji wakivunjika mbavu kwa kucheka!

 

“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic Bongo, siku zote imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunatoa msisitizo kwenye maudhui yandani na vichekesho hivi ya Mwantumu ni mfano halisi. Hii ni yetu, imetengenezwa hapa tanzania na wazalishaji, waandaaji na waigizaji wote wa hapahapa nchini” alisema Alpha.

 

Vichekesho vya Mwantumu vilianza msimu wa kwanza mnamo Oktoba 2017 Na kuendelea kwa muda wa mwaka mmoja ambapo vilikuwavikionyeshwa mara moja kwa wiki. Katika msimu huu mpya vichekesho hivyo vitaonekana mara mbili kwa wiki siku ya  Jumanne na  Jumatano  saa mojana nusu usiku. Hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi kwani kumekuwa na maombi mengi yakuongeza vipindi hivyo kutokana na umaarufu wake.

 

About Alex

Check Also

Capture

STARTMIMES YAJA NA LIPA TUKUBUSTI MSIMU WA KRISMASI

Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 + 20 =