Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / Arif Abri Apongezwa na Wazazi CCM Iringa kwa kusaidia CCM

Arif Abri Apongezwa na Wazazi CCM Iringa kwa kusaidia CCM

IMG_20181016_123559
Mwenyekiti wa jumuiya ya  wazazi wa  chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa vijijini  Marco Kihongo (kushoto)  akipokea msaada wa fedha  kiasi  cha shilingi milioni 1  kwa ajili ya ununuzi wa kadi  za chama ,kutoka kwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  Arif Abri 
IMG_20181016_123853
  katibu  mstaafu wa CCM wilaya ya Iringa vijijini  Dodo  Sambu (kulia )  akimpongeza mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa anayewakilisha  wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri kwa  kusaidia jumuiya ya  wazazi na  chama 
IMG_20181016_124036
Mjumbe wa  mkutano mkuu wa CCM Taifa Arif Abri  katikati akiwa na  viongozi wa jumuiya  za CCM na  katibu mstaafu wa  CCM wilaya ya Iringa vijijini Dodo Sambu (mweye shati la kijani )
……………………….
JUMUIYA  ya  wazazi wa chama  cha mapinduzi  (CCM)  wilaya ya  Iringa  vijijni mkoani Iringa  kimepongeza  jitihada mbali mbali  zinazofanywa na mjumbe wa  mkutano  mkuu wa CCM Taifa  anayewakilisha  wilaya ya  Iringa vijijini Arif Abri katika  kuiwezesha  jumuiya  hiyo  kuwa na miradi yake .
Mwenyekiti  wa  jumuiya  hiyo Marco Kihongo ametoa  pongezi  hizo  leo    wakati akipokea  pesa  kiasi cha shilingi milioni 1 kutoka kwa  mjumbe  huyo kwa ajili ya kutekeleza  ahadi yake aliyoitoa kwa jumuiya  hiyo   ya  kuchangia  pesa hizo kwa ajili ya  ununuzi wa kadi  za jumuiya kwa  wanachama  wapya.
Kihongo alisema  kuwa mchango huo  wa  fedha  ni mtaji mkubwa kwa  jumuiya  hiyo kuweza kuongeza idadi kubwa  zaidi ya  wanachama wake  na  kuwa zoezi la  uongezaji  wanachama  litaanza mara moja  kuanzia sasa .
Huku  katibu  wa  jumuiya   hiyo  Martin Mfala alisema  pamoja na mjumbe  huyo  kuchangia  kiasi hicho  cha fedha  pia aliwaagiza  kutafuta  mashamba  kwa  ajili ya  kupanda  miti pamoja  mbali mbali  ikiwemo ya korosho katika  tarafa ya  Idodi na  kuwa  tayari wamefanikisha kupata ardhi kwa  ajili ya  kununua na  kukodi kwa kupanda miti hiyo .
Hivyo alisema  iwapo  watafanikiwa  kupata  ardhi  hiyo wataweza kupanda miti ambayo itakuwa ni sehemu ya miradi ya  jumuiya ya  wazazi katika wilaya  hiyo  huku akiomba  kusaidiwa  kutengeneza  pikipiki mbili za jumuiya hiyo ambazo kwa  sasa ni mbovu kwa  ajili ya  kusaidia  usafiri  wa  kwenda  kutembelea miradi ya  jumuiya .
Awali  mwanachama  wa  CCM wilaya ya  Iringa vijijini Thom Malenga  ambae ni katibu wa mbunge wa jimbo la Ismani ,Wiliam Lukuvi alisema  kuwa  jitihada kubwa  zimekuwa  zikifanywa na  Arif Abri katika  wilaya ya  Iringa  ni mfano wa kuigwa na  kuwa kazi mbali mbali amekuwa  akichangia  hivyo  kuchangia fedha  hiyo ni mwendelezo wa misaada mbali mbali ambayo amekuwa akitoa.
”  Tunaamini Mungu  humjalia   zaidi  yule anayetoa kwa  ajili ya  wengine  kifupi  tunashukuru  sana  kwa  misaada  mbali mbali ya kijamii na  chama katika  wilaya  ya Iringa vijijini ”  alisema Thom 
Akikabidhi  fedha   hizo  Arif  alisema  pamoja na  kuwa amefanya kazi na makatibu  wengi  wa  wilaya ndani ya  wilaya  ya  Iringa vijijini  ila utendaji kazi wa katibu Dodo Sambu ambaye  kwa  sasa ni mstaafu amekuwa  mchapakazi  sana na kw  muda wa miaka  mitatu aliyokuwepo  Iringa kazi yake imeonekana.
Hivyo  amesema  mategemeo yake  ni kwa katibu  ajaye  kuendeleza  umoja na mshikamano  uliokuwepo kamanguvu ya  ujenzi wa chama hicho katika  wilaya ,mkoa na Taifa  ili  ushindi wa CCM uzidi  kuongezeka  daima.
” Jana  wakati namtafuta  katibu wa jumuiya ya  wazazi  nilimpigia  mwenyekiti wa  umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Iringa vijijini ambae pia  aliomba kusaidia  pikipiki  nilimuahidi kuwa asiwe na hofu  nitampa  pikipiki   hiyo nilitegemea  leo kuja kukabidhi hapa  ila kasema yupo nje  ya mji kikazi  sasa  akirudi nitamkabidhi ”  alisema Arif 
Kuwa maombi ya jumuiya ya  wazazi kuhusu kutengenezewa   pikipiki  mbili atayafanyia kazi  haraka pamoja na  utengenezaji wa gari la  chama  wilaya .
Mjumbe  huyo pia alisema  juu ya mradi wa shamba atalitekeleza kwa  kununua shamba hilo  lenye ukubwa wa hekari 20  kama  mradi na  kuwa  pamoja na  miradi hiyo  pia umoja wa  wanawake   Tanzania (UWT) wilaya ya  Iringa nao  watasema  wanahitaji nini  ili wasaidiwe .
” Nataka  kuwaeleza kuw  katika familia  yangu  mimi  kutoka babu zangu   wote ni CCM na tunaipenda sana  CCM na  tupo tayari kuendelea   kusaidia  uhai wa chama ili kuona  CCM inaendelea  kutawala  daima” alisema Arif Abri .
Akishukuru  kwa misaada  hiyo katibu mstaafu wa CCM wilaya  ya  Iringa vijijini Dodo Sambu alisema  kuwa heshima   na ushindi wa CCM wilaya ya  Iringa  vijijini na mjini imetokana na jitihada za mjumbe   huyo wa mkutano mkuu wa CCM Taifa  kupitia  wilaya ya Iringa vijijini  pamoja na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) anayewakilisha mkoa wa Iringa Salim Asas ambao  wamekuwa  wakijitoa kwa nguvu  zote .

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 + 11 =