Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / MKOA WATILIANA SAINI NA KAMPUNI YA KUSAMBAZA VIFAA TIBA NA DAWA

MKOA WATILIANA SAINI NA KAMPUNI YA KUSAMBAZA VIFAA TIBA NA DAWA

kwitega

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali ya mkoa wa Arusha Leo,jana imetiliana sahihi na Kampuni ya Planet
Pharmaceutical Ltd, ya mkoa Dar es salaam kwa ajili ya kutoa huduma za
vifaa tiba na madawa kama muungozo wa wizara ya Afya maendeleo ya
jamii wazee na watoto ilivyotoa.

Akitiliana sahihi na kampuni hiyo Katibu tawala wa mkoa wa Arusha
Richard Kwitega alisema kuwa hii ni hatua kubwa kwa mkoa wetu kwa sasa
hakuta kuwa na upungufu wa dawa baada ya kumpata mshitiri huyu.

Amesema kuwa mkataba huo umeambatanisha pamoja na bei utaenda hadi
kwenye hospitali zetu mkoani hapa sanjari na vituo vya Afya na
zahanati kwa kuweza kuagiza moja kwa moja dawa na vifaa vyote vya
matibabu kutoka kampuni hiyo.

“Mchakato huu ulianza toka mwezi Mei mwaka huu kwa kutangaza zabuni
hadi kupatikana kwa mshitiri huyu na leo ndio tunatiliana sahihi ili
kuanza kazi ya kuhudumia kwenye hospitali zote za mkoa wetu”alisema
Kwitega.

Kwa Upande wake Afisa Manunuzi na Ugavi Mkuu mkoani hapa Elirehema
Masanja amesema kuwa mchakato huo ulianzia mwezi mei nmwaka huu na
wamepata mshitiri kampuni ya Planet Pharmaceutical yanye makao makuu
jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa huduma za vifaa tiba na dawa
kwa hospitali za serikali vituo vya Afya na zahanati zote mkoani hapa.

Alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kushinda zabuni hiyo na itatakiwa
kuanza mara moja kazi hiyo baada ya utiliaji saini huo ikiwemo kutoa
huduma za usambazaji wa vifaa tiba na madawa yanaokosekana kwenye
vituo vyetu vya Afya hapa mkoani mwetu.

Ne Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Venu Madhav alisema kuwa kampuni hiyo
inauzoefu mkubwa wa kazi hiyo ambapo imekuwa ikifanyakazi hizo kwenye
mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Shinyanga na sasa wamekuja Arusha na
wamejipanga kutoa huduma yenye tija kwa hospitali zetu mkoani hapa.

Amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa hudma bora na
vifaatiba vyeny ubora unaokubalika kwani kampuni hiyo inauzoefu wa
muda mrafu katika masuala hayo hapa nchini na nje ya nchi.

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 + 10 =