Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / ZIARA YA DC MJEMA, ILALA; YAACHA NEEMA KWA MADEREVA BAJAJI

ZIARA YA DC MJEMA, ILALA; YAACHA NEEMA KWA MADEREVA BAJAJI

1

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema leo ameanza ziara yake katika Jimbo la Ilala, ambapo ametembelea soko la Samaki Ferri na kufanya vikao katika zone zote za Soko hilo ili kujionea shughuli za wavuvi na mama lishe, kusikiliza kero zao na kutoa maelekezo ya utatuzi wa kero hizo.

index

Aidha Mjema alifanya mkutano wa hadhara ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao. Pamoja na mambo mengine Mjema amepiga marufuku bajaji zote ambazo zinaendashwa na madereva wasio walemavu kufika mjini na kwamba ruksa hiyo imetolewa kwa madereva walemavu tu, ikiwa ni hatua ya serikali katika kutengeneza fursa kwa walemavu hao.

2

Kesho ziara ya Mkuu wa Wilaya itaendelea katika kata za Mchafukoge, Upanga Mashariki, Magharibu na Jangwani. Katika ziara hiyo Mhe. Mjema anaambatana na wataalamu mbalimbali ambao hutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayoulizwa na wananchi. Ziara hii inalenga kuwasogezea karibu wananchi serikali yao kwa kupunguza kero mbalimbali zinazowakabili.

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini¬† vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 − 9 =