Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA YA MATUKIO YA KIHALIFU KUTOKA JESHILA POLISI MKOANI MBEYA

TAARIFA YA MATUKIO YA KIHALIFU KUTOKA JESHILA POLISI MKOANI MBEYA

Gari iliyokuwa imebeba vifaranga toka nchi jirani ikiwa Kituo cha Polisi Tukuyu

Mnamo tarehe 16.10.2018 majira yaa saa 21:30 usiku huko eneo la Mpandapanda lililopo Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya katika baràbara kuu ya Mbeya kwenda Tukuyu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata watu watatu ambao ni:-

  1. BOAZ MWAKIFUMBWA [51] Mkazi wa Airport – Mbeya,
  2. RAYMOND MNOSI [42] Mkazi wa Tegeta – Dsm
  3. EMANUEL ELIA [37] Dereva na Mkazi wa Nsalala – Uyole

Watuhumiwa walikamatwa wakiwa na gari lenye namba za usajili T. 322 DNW aina ya Toyota Coaster wakiwa wamebeba vifaranga vya kuku kutoka nchini Malawi boksi 147 huku kila boksi likiwa na vifaranga 100 na kufanya jumla ya vifaranga hivi kuwa 14,700.

KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI (GONGO) NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

Mnamo tarehe 16.10.2018 majira ya saa 16:58 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko Kijiji na Kata ya Mwaya, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya  Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la ATUPELE MWAKALUKWA [38] Mkazi wa Mwaya akiwa na pombe haramu ya Moshi @ gongo lita 15.

Aidha katika upekuzi zaidi, mtuhumiwa alikutwa akiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku na Serikali aina ya Win boksi 05 na Charger boksi 3 kutoka nchini Malawi. Pia mtuhumiwa alikutwa na dawa za kulevya aina ya bhangi kilo 4 na gram 445 katika kibanda chake cha biashara.

Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya shauri hili kukamilika.

KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Mnamo tarehe 16.10.2018 majira ya saa 14:00 mchana Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko katika Kijiji cha Bitimanyanga, Kata ya Mafyeko, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye ANTONY SAMWEL [25] Mkazi wa Bitimanyanga akiwa na bhangi kilo 5.

Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi na atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni za barabarani hasa katika maeneo tete yenye milima na miteremko mikali, Igawilo, Kawetele, Nyoka na mlima Iwambi ambapo magari ya abiria na madogo yanapita tofauti na magari makubwa ya mizigo. Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na ukaguzi katika nyumba za kulala wageni ili kukabiliana na uhalifu/wahalifu.

Imesainiwa na:

[MODESTUS CHAMBU – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Kamishna Msaidizi wa Polisi – MODESTUS CHAMBU – 0658 376 052

Mwandishi wa RPC – 0652 343 929

Mabox yenye vifaranga yakiwa kwenye gari Zoezi la kushusha mabox yenye vifaranga vya kuku likiendelea Kituo cha Polisi Tukuyu

About bukuku

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty + six =