Tuesday , January 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / MILIONI 500 ZATUMIKA KULETA NEEMA YA MAJI CHARAMBE NA KIBONDEMAJI

MILIONI 500 ZATUMIKA KULETA NEEMA YA MAJI CHARAMBE NA KIBONDEMAJI

1

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

2

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akikata utepe kuzindua miradi ya maji Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam.

3

Afisa Mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian  Luhemeja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

4

Sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso  ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

5

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizindua mradi hou Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.

(Picha zote na DAWASA)

………………………..

Na; Mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameikabidhi DAWASA miradi miwili ya majisafi na usafi wa mazingira yenye thamani ya milioni 500 na inahudumia wananchi wasiopungua 160,133 lengo likiwa kuwafikia wananchi 280,000 katika Wilaya ya Temeke.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri Mhe. Aweso amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa kufikia mwaka 2020.

“Mradi  huu wa majisafi una uwezo wa kuzalisha lita laki 224,000 za maji kwa siku na utahudumia wakazi wa Charambe na Kibonde maji katika Manispaa ya Temeke ambapo wananchi wameanza kuunganishiwa huduma hii ya maji kupitia  Ofisi ya DAWASA Temeke”. Alisisitiza Mhe. Aweso

Kuanza kwa mradi huu kunasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo na kuchangia  katika kukuza shughuli za uzalishaji na maenedeo katika maeneo hayo.

Kwa upande wa mradi wa kuchakata  majitaka Mhe. Aweso amebainisha kuwa mradi huo una uwezo wa kuchakata lita 50,000 za majitaka kwa siku ambapo mradi huo utasaidia upatikanaji  wa mbolea, maji kwa ajili ya umwagiliaji, pamoja na gesi.

DAWASA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika  kuimarisha huduma zake ikiwemo kudhibiti uvujaji wa maji na kuweka mtandao mpya katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya majisafi na salama.

 

About Alex

Check Also

_MG_9933

CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE WA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-,PANGANI HADI BAGAMOYO

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × three =