Thursday , March 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / IGP SIRRO AONYA VIKALI WANAOHUSIKA NA MATUKIO YA UTEKAJI, ASEMA POPOTE WATAKAPOKIMBILIA HAWAKO SALAMA

IGP SIRRO AONYA VIKALI WANAOHUSIKA NA MATUKIO YA UTEKAJI, ASEMA POPOTE WATAKAPOKIMBILIA HAWAKO SALAMA

1

Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akionyesha mbele ya waandishi wa habari  moja ya silaha ya kivita AK 47 iliyopatikana kwenye garilililohusika katika utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji Oktoba 11  2018 mwaka huu katika hoteli ya Collesium jijini Dar es salaam.

2

Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akionyesha mbele ya waandishi wa habari  moja ya silaha mbili  aina  ya Bastola  ziliyopatikana kwenye gari lililohusika katika utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Collesium jijini Dar es salaam.

3

Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Saimon Sirro akionyesha mbele ya waandishi wa habari  moja ya Bastola tatu ziliyopatikana kwenye gari lililohusika katika utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji Oktoba 11 mwaka huu katika hoteli ya Collesium jijini Dar es salaam.

4

Hizi ndiyo silaha AK 47 moja na bastola tatu zilizopatikana kwenye gari lililohusika katika tukio la utekaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji hivi karibuni jijini Dar es salaam.

5

Gari lililohusika katika utekaji huo lililokutwa eneo la Gymkana jijini Dar es salaam.

6

…………………………………………………………………

KAMANDA wa Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa baada ya kupatika kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji Moo.Jeshi la polisi linaendelea na msako kuhakikisha waliokuwa wamemteka mfanyabiashara huyo wanapatikana popote walipo.

Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha watekaji hao wanapatikana wakiwa hai au wamekufa huku akitoa onyo kali kwa vikundi ambavyo vinaingilia majukumu ya jeshi hilo nakubainisha kwamba anamashaka na uraia wao.

IGP Sirro ameyasema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya  Jeshi la Polisi ambapo amesema katika kuhakikisha wanapoteza ushahidi walijaribu kuliunguza Gari hilo ambalo lilikuwa limetelekezwa katika eneo la Ghymkana.

Amesema taarifa za kupatikana kwa Mohamed Dewji  zilitolewa na  Askari wa Getini katika eneo hilo la  Ghykhana  ambapo Mo alimtaka Askari huyo kutoa taarifa kwa  familia yake ndipo walipokuja katika eneo hilo.

Amesema kuwa baada ya kuja katika eneo hilo ndipo walipojulishwa Polisi nawenyewe kufika katika eneo la tukio na kujirisha kupatikana kwa Mfanyabiashara huyo Dewji.

“Ilikuwa majira ya saa saba usiku Maeneo ya Gymkhna gari aina ya Toyota Sulf  Lilitelekezwa ndani yake likiwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji ambapo baada ya kumwacha katika eneo hili walijaribu kutaka kupoteza ushahidi kwa kulichoma moto gari ambalo lilimbeba.” amesema Sirro.

Akifafanua zaidi amesema Gari hilo ni lile ambalo alilionyesha mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii.gari lenye namba za usajiri  T314AXX Na kwenye vioo vya pembeni kulikuwa na namba za usajili AGX 404 MC yenye rangi ya blue nyeusi na ufito wa rangi ya shaba kwa chini.

Kamanda Sirro amesema kuwa baada ya kufanya mazungumzo na Mo Dewji aliwaeleza waliomteka walikuwa wanazungumza lugha ya kingereza na mmoja lugha ya kiswahili cha hovyo.

Kwamujibu wa kamanda sirro amesema Mo aliwaeleza kuwa baada ya kumteka walitaka atoe fedha ambapo aliwaeleza yeye alikuwa hana hela na badala yake aliwaeleza awape namba za simu za baba yake.

Amesema hata walipopewa na za simu za baba yake hawakuweza kumpigia bila shaka waliogopa mtego wa polisi hivyo.” Sisi kama polisi tunashukuru Mo kapatikana lakini Jeshi la Polisi tutaendelea na msako na tunawataka wananchi.kuendelea kushirikiana nasi ili kuhakikisha tunakomesha matukio haya.”amesema Sirro.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa atahakikisha waliomteka Mo Dewji wanakamatwa .tena wakiwa hai au wamekufa ili kukomesha vitendo.hivi na taifa kuendelea kuwa mahala salama wakati wote.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro ametoa Onyo kali kwa kikundi cha baadhi ya watu ambao wanaingilia utendaji wa Jeshi la Polisi kupitia mitandao ya kijamii.

” Kuna kikundi ambacho chenyewe kipo kwa ajili ya kuingili majukumu ya polisi jamani Polisi wanafanya kazi usiku kucha tena wakipita kukagua katika kila eneo nakwamba wenyewe wamelala na wake zao lakini kazi yao kuingilia kazi za polisi.”amesema Sirro.

Pia amezitaja baadhi ya nchi ambazo wanashirikiana kuhakikisha watekaji wanatiwa nguvuni.ambazo ni Afrika kusini,kenya,Uganda,Msumbini,…nakwamba ndani ya siku tisa askari wake hawajalala kuhakikisha Mo anapatikana.

Mo Dewji alitekwa Oktoba 11,2018 majira ya alfajiri katika Hoteli ya Colessum iliyopo masaki ambapo mara zote amekuwa akifanya mazoezi ya Gym.

About bukuku

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 13 =