Thursday , March 21 2019

Home / BIASHARA / KAMISHNA WA TRA AFUNGUA FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

KAMISHNA WA TRA AFUNGUA FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI

1

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akifungua Fainali za Mashindano ya Vilabu vya Kodi katika shule za sekondari za Dar es salaam na Pwania Pwani zinazofanyika katika Chuo cha Kodi Mwenge jijini Dar e salaam, Katika mashindano hayo wanafunzi kutoka shule mbalimbali wanashiriki ili kujenga ufahamu weledi wa faida ya kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kutoa risiti na kudai risiti wakati watu wanapofanya manunuzi.

2

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato TRA Bw. Charles Kichere ili kufungua fainali hizo.

3

Baadhi ya maafisa elimu na wageni kadhaa kutoka taasisi mbalimbali  walioshiriki katika fainali hizo ili kushuhudiajinsi wanafunzi wanavyoshindana.

4

Majaji wa mashindano hayo wakiwa tayari kwa kufanya uamuzi kwa kadiri watakavyoona ni shule gani imefanya vizuri katika fainali hizo.

5

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere  akiwa  pamoja na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo katika fainali hizo.

6 7

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoa wa Dar es salaam na Pwani.

8

Wanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Migombani.

9 10

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari ya Turiani.

11

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam na Pwani wakiwa katika fainali hizo.

…………………………………………………………………

Na Veronica Kazimoto- Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amefungua fainali za mashindano ya kumi na moja (11)  ya vilabu vya kodi katika Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yaliyofanyika leo katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa,  Kichere amesema lengo la mashindano hayo ni kuwafundisha wanafunzi uzalendo na kukuza uelewa wao juu ya masuala mbalimbali ya kodi ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari.

“Haya mashindano yanafanyika kama sehemu ya kujenga uzalendo kwa wanafunzi wetu ili waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na hatimaye waweze kulipa kodi kwa hiari maana tunasema samaki mkuje angali mbichi,” alisema Kichere.

Ameongeza kwa kusema kuwa, “Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania tunasema kwamba elimu ndio kitu muhimu sana kwasababu watu wakielewa umuhimu wa kulipa kodi, tutakusanya kodi nyingi zaidi ambazo hutumika katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, utoaji wa elimu bure, uboreshaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya maabara na kufundishia.”

Aidha, Charles Kichere amebainisha kuwa, Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali inafanya mpango wa kuingiza mtaala wa somo la kodi kuanzia Shule za Msingi hadi vyuoni ili kujenga uzalendo wa kulipa kodi kwa hiari nchini.

Mamlaka ya Mapato Tanzania ilianzisha vilabu vya kodi mwaka 2008 na mpaka sasa kuna jumla ya vilabu 226 Tanzania Bara vikiwa na jumla ya wanafunzi 27,250 ambao ni wanachama hai wa vilabu hivyo.

Mashindano ya mwaka huu yameshindanisha jumla ya shule 50 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambapo shule 28 zimeingia fainali zikiwa zimegawanyika katika makundi mawili, shule 18 zinashindana katika kujibu maswali wakati shule 10 zinashindana kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusu kodi.

About bukuku

Check Also

maxresdefault

HOTELI YA KWANZA ARUSHA YATENGA MILIONI KUMI KWA AJILI YA YATIMA

UONGOZI wa hoteli ya kitalii ya New Safari Hoteli ya jijini Arusha umefanikiwa kujiwekea utaratibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × 4 =