Tuesday , January 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAKAZI WA VIJIJI KUMI NA MBILI WANAOZUNGUKA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA NGEZI VISIWANI PEMBA WAANZA KUNUFAIKA NA MATUMIZI YA MAJIKO

WAKAZI WA VIJIJI KUMI NA MBILI WANAOZUNGUKA MSITU WA HIFADHI YA SERIKALI WA NGEZI VISIWANI PEMBA WAANZA KUNUFAIKA NA MATUMIZI YA MAJIKO

885-768x512

Na Masanja Mabula –Pemba

WAKAZI wa vijiji kumi na mbili vinavyozunguka hifadhi ya msitu wa Serikali wa Ngezi kisiwani Pemba wameanza kunufaika na matumizi ya majiko ya mkombozi kutoka Jumuiya ya Vijana Tumbe yanayotumia kuni kidogo.

Utumiaji wa majiko hayo utasaidia kudhibiti vitendo vya  hujuma ndani ya hifadhi hiyo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wanaotafuta mahitaji ya kuni.

Jumla ya majiko sitini yatajengwa katika baadhi ya familia za vijiji hivyo , ambapo wananchi wengine wapata taaluma ya ujenzi wake katika familia zilizobahatika kujengewa.

Baadhi ya akinamama waliozungumza na mwandishi wa habari hizi , wamesema kuwa majiko hayo yatapunguza matumizi ya kuni na hivyo kupunguza athari za uharibifu wa mazingira ndani ya hifadhi.

Asha Omar mkaazi wa shehia ya Tondooni moja ya kijiji kinachozunguka hifadhi hiyo, amesema kabla ya kuanza kutumia jiko hilo, alikuwa anatumia kuni zaidi ya ishirini kwa kupikia na hivyo kumfanya kila siku aingie ndani ya hifadhi kukata kuni.

“Jiko hili ni mkombozi kama lilivyo jina lake, tangu nianze kulitumia , nimepungua kwenda msituni mara kwa mara kwani natumia kuni kidogo kuliko hapo kabla sijaanza kutumia ”alieleza.

Amefahamisha kuwa , katika kijiji chao kunakawaida ya akinamama  kujifunza kutoka kwa wenzao, hivyo anaaamini kwamba elimu ya ujenzi wa majiko hayo itasambaa katika familia zote.

Naye salma Busagala Dida amesema kuwa kutokana na jamii ya vijiji  hivyo kuhamasika kutunza mazingira ya msitu, ni dhahiri kwamba  watatumia fursa kuhajihishana kujenga majiko hayo.

Akizungumza nyumbani kwake , Salma amesema wananchi kutumia taaluma hiyo ili hifadhi yam situ wa Ngezi, iendelee kutumika katika kuchangia uchumi wa nchi na wananchi wake.

Aidha Salma amesema mbali na kupunguza matumizi ya kuni , lakini majiko hayo pia yatasaidia kuzuia ajali za moto hasa kwa watoto wadogo.

“Kiukweli majiko haya pia yatapunguza ajali za moto zinazotokea wakati wa kupika kutokana na jinsi lilivyojengwa limehifadhiwa vizuri haliwezi kutoa moto wenye madhara kwa mpikaji”alifahamisha.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Tumbe Omar Juma Seif amesema uwamuiz wa kujenga majiko hayo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya kuulinda Msitu wa Ngezi ambao ni chanzo cha mapato cha Serikali.

“Tumeona iko haja kwa wakaazi wa vijiji vinavyozunguka msitu wa Ngezi kuwawezesha kwa kuwajengea majiko yanayotumia kuni kidogo ili kupungua hujuma ndani ya hifadhi”alieleza.

Katibu wa Jumuiya hiyo Omar Ali Amour amefahamisha kwamba tayari wameshajenga majiko 20 , ambapo bado wanaendelea kujenga mengine katika familia ya shehia ya Tondooni na Makangale.

Afisa Mkuu wa Hifadhi ya Msitu wa Ngezi Abdi Mzee Kitwana amepomngeza uwamuzi uliochukulia na Jumuiya hiyo na kusema kwamba utasaidia kupunguza uvamizi ndani ya msitu huo.

About Alex

Check Also

_MG_9933

CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE WA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-,PANGANI HADI BAGAMOYO

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza na waandishi wa habari …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 3 =