Thursday , March 21 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI MKUU KUFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA AZAKI JIJINI DODOMA

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MAONESHO YA WIKI YA AZAKI JIJINI DODOMA

kasimu+pic

Waziri  Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufungua maonyesho ya wiki ya Asasi za kiraia jijini Dodoma kesho Washiriki 800 kutoka asasi za Kiraia zaidi ya 250 watashiriki , kuanzia Oktoba 22 hadi 26 mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji wa The Foundation For Civil Society, Francis Kiwanga alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuonyesha mafanikio ya shirika hilo katika maendeleo ya Taifa.

Alisema kuwa The Foundation For Civil Society imepata mafanikio mengi hapa nchini katika maeneo mbalimbali ya kimaendeleo huku akisema kuwa asasi nyingi zimejitahidi kufanya vizuri na kutimiza malengo ya kusaidia jamoo

Kiwanga alisema kuwa katika maonyesho hayo wanatarajia kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kuziwesha jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo masuala ya utawala bora na uwajibikaji.

Alisema kuwa mpaka hivi sasa wanafanya kazi na Asasi zaidi ya 150 nchini ambazo wanaziwezesha katika kuzipatia ruzuku.

Aidha alisema kuwa katika maonyesho hayo pia wataangalia namna gani wanaweza kushiriki katika kuchangia katika mkakati wa Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.

“Pia maonyesho haya tutayatumia kuwa karibu na viongozi wa serikali, bunge, taasisi binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu nini tunafanya na kuondoa dhana iliyopo ya kuwa sisi tupo kwajili ya manifaa yetu”alisema.

Alifafanua kuwa hivi sasa wameweka mikakati ya kuhakikisha kila fedha inayotolewa kama ruzuku kwa asasi mbalimbali zinatumika ipasavyo.

“Sasa hivi tumeweka mikakati kila fedha ianyotoka kama ruzuku lazima itumike vizuri na mashirika mengi yameweza kufanya vizuri kwa asilimia kubwa lengo letu sio kujinufaisha sisi”alisema.

Mbali na mambo mengine Kiwanga alisema kuwa asasi zinalenga kuhakikisha wanakuwa karibu na serikali katika kufanya maendeleo na kutoa ushauri kwa serikali kwa nia ya kuboressha sera mbalimbali za kimaendeleo pale inapobidi.

“Asasi za kiraia siyo adui wa serikali kazi kubwa ni kupeleka mkono pale ambapo serikali haijafika na jambo kubwa zaidi ni kuchochea maendeleo kwa jamii nzima kwa na makundi mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa kama vile makundi ya watu maalum na wenye mahitaji maalumu ili waweze kutambua haki zao na kupata haki zao” alisema Kiwanga.

Pamoja na maonesho hayo kutakuwepo na maonesho mbalimbali pamoja na utoaji wa elimu kwa Umma hususani uelimishaji kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda pamoja na utoaji huduma ya msaada wa kisheria.

Kwa upande wa  Racheli Chagonja alisema kuwa kutakuwepo utoaji wa elimu juu ya matumizi ya mafuta,madini na gesi na kuhamasisha wananchi kuweza kutumia rasilimali walizomazo kwa faida ya kimaendeleo na kuona umuhimu wa kuwa na Tanzania ya viwanda kama kauli mbiu ya serikali inavyoeleza.

Alisema kuwa elimu inayotolewa kwa jamii sambamba na ushauri wa kisheria ni huduma ambayo inatolewa bure bila kutoza fedha ya aina yoyote ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wananchi kujua fursa ambazo wanatakiwa kuzitumia.

About Alex

Check Also

IMG_7568

Lishe Endelevu kumaliza Tatizo la Udumavu Mkoa wa Rukwa

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akitoa nasaha wakati wa kufungua kikao cha …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 2 =