Tuesday , January 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / MAHAFALI YA 41 SHULE YA SEKONDARI SINGE HAIJAWAHI KUTOKEA

MAHAFALI YA 41 SHULE YA SEKONDARI SINGE HAIJAWAHI KUTOKEA

MKUU WA WILAYA YA BABATI

Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati  Elizabeth Kitundu,  amewataka wahitimu wa kidato cha nne kuachana na vishawishi vyote ambavyo vitawapelekea kushindwa  kufikia ndoto zao.

Wahitimu wakiimba wimbo wa Taifa

Kitundu  ametoa wito huo katika sherehe za mahafali ya 41  ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Singe iliyopo kata ya Singe mjini Babati inayomilikiwa na Jimbo katoliki la Mbulu,ambapo alisema katika mafanikio lazima kuongeza bidii sambamba na kuachana na vishawishi vya aina zote ambavyo vitawafelisha  kufikia malengo waliyojipangia.

MKUU WA WILAYA YA BABATI

Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa bado kazi ya kusoma wanayo ambayo ni kazi ngumu na kuwataka waongeze jitihada kwani hakuna kazi ngumu kama kusoma lakini akawasibitishia kuwa wataiweza licha ya ugumu uliopo.

Alisema kuwa Serikali imechukua uamuzi wa makusudi wa kutangaza elimu bila malipo kwa lengo la kuwataka vijana wote wenye uwezo na wasio na uwezo waweze kusoma na kupata elimu inayohitajika.

Alisema  anatamani shule za Babati zifanye vizuri kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita isiwepo division 0 wala Division 3 na 4 akiitaka Singe iwe ya Mfano.

Akizungumzia kuhusu walimu,alisema serikali haitokuwa tayari kufumbia macho  walimu wanaofanya vitendo vya aibu kwa wanafunzi wao wanaowafundisha.

Wahitimu wakipiga tarumbeta na band yao ya Shule

Aidha amewaasa wasichana wa kike wajitambue huku akiwageukia wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kufuatilia mwenendo wa  masomo yao kabla na baada ya likizo.

Kwa upande mwingine amewataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.

Nae Mkuu wa shule ya Sekondari Singe Brother John Kihaumbi,amesema katika shule yao wamehakikisha wanakuwa na walimu wenye uwezo katika ufundishaji,vifaa vyote vinavyohitajika vya nadharia na vitendo ili kuwasaidia wanafunzi  kupata mafunzo ambayo yatawasaidia katika maisha yao baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari.

Ameongeza kuwa,  sio kila mtu anaweza kuwa mwalimu kwani wengine wanashindwa kusimamia vyema taaluma hiyo hali inayowarudisha wanafunzi wengi nyuma.,fani hii imeingiliwa sana na watu ambao hawana maadili ya ualimu, na matokeo yake idadi kubwa ya vijana hawaendelei na elimu ya juu.

Wahitimu

Mkuu huyo ameiomba serikali ikae chini na kuangalia upya mitaala inayotumika kwa sasa kulingana na hali halisi na  mahitaji ya sasa ili mwanafunzi anapohitimu elimu ya Sekondari awe na ujuzi utakaomsaidia katika maisha yake na sio kuwa tegemezi kwa wazazi.

“Hatutegemei kuwaona vijana wetu waliomaliza kidato cha nne wawe wapiga debe kwenye vituo vya mabasi au wacheza kamari huko mitaani bali tunataka elimu walioipata iwasaidie kuwaingizia kipato halali na kuwa raia wema wa Tanzania”alisema Brother John.

Brother John amewaaambia wahitimu hao kuwa wasome ujumbe wa neon la Mungu kutoka katika Biblia katika kitabu cha Waefeso 3:12-13 ambapo mtakatifu Paulo alisema, Hajamaliza mambo yote anaanza tu ,hivyo  kidato cha nne sio mwisho wa elimu bali wanapaswa kuongeza bidii zaidi na kuendelea na masomo ya A Level na hatimaye chuo kikuu ili kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.

Aidha Brother John  akizungumzia muhula mpya wa Masomo,aliwaomba  wazazi na walezi wenye watoto wanaotarajia kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 kwenda kuchukua fomu zaa kujiunga na shule hiyo kongwe mkoa wa Manyara ili kumsaidia mtoto kufikia malengo yake ya kupata elimu Bora.

Naye mwanafunzi Mohamedi Juma aliehitimu kidato cha sita shuleni hapo na  kuwa mwanafuzi bora Kitaifa kwa kupata madaraja ya juu,akawatia moyo wahitimu kwamba wasome kwa bidii na kuwatumia vizuri walimu,Wawe na moyo wa kujituma kwa sababu kusoma sio jambo rahisi hata kidogo.

Mwanafunzi aliefanya vizuri kidato cha sita Kitaifa Mohamedi Juma akipeana mkono na Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu.

Jumla ya Wahitimu 215 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Singe yenye mchepuo  wa masomo ya Sanaa wanatarajia kufanya  mitihani yao ya mwisho mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Shule ya Singe ilianzishwa mwaka 1974 kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na hatimaye kidato cha tano na sita mwaka 1995 ikiwa kama shule ya kati Ya Serikali na baadaye wakaamua kuiachia taasisi ya dini [Roma Catholic] kuiongoza mpaka sasa.

Katika mji wa Babati,Shule ya Sekondari Singe ndio shule ambayo kila mwaka hujaza mamia ya watu katika Mahafali ya Kidato cha nne kutokana na Shamra shamra na maandalizi mazuri yanayofanywa.

About Alex

Check Also

PICHA 2 -min

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA UKUSANYAJI MADUHULI

Na Asteria Muhozya, DODOMA Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × three =